MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua siku za wiki katika mawasiliano ya kila siku
- kutaja majina ya siku za wiki kwa mfululizo ili kumsaidia kuratibu shughuli za siku,
- kuelezea shughuli za siku mbalimbali za wiki ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kutumia majina ya siku za wiki kutunga sentensi ili kuimarisha mawasiliano,
- kuthamini kila siku ya wiki ili kutilia maanani shughuli za siku husika maishani.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atambue siku za wiki yaani: Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa kutumia kadi za maneno.
- Mwanafunzi aweza kuimba wimbo wa siku za wiki.
- Mwanafunzi aweza kukariri mashairi kuhusu siku za wiki.
- Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano ya shughuli za siku za wiki k.m. Jumatatu naenda shule, Ijumaa, Jumamosi au Jumapili nashiriki ibada n.k.
- Wanafunzi waweza kupanga kadi za majina ya siku za wiki kwa utaratibu wakiwa wawili wawili.
MASWALI DADISI
- Wiki moja ina siku ngapi?
- Unaenda shule siku gani?
- Unaweza kutaja na kuandika
majina yapi ya siku za wiki kwa mfuatano?
4) Waweza kutumia majina yapi ya siku za wiki katika sentensi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kazi za vikundi ujuzi wa kidijitali : kuandika kwa vipakatalishi na kusikiliza visa ubunifu: kueleza namna ya kutumia kila siku aliyo nayo.
Uhusiano na masuala mtambuko: stadi za Maisha (uwajibikaji) -kufanya uamuzi wa jinsi ya kutumia siku za wiki uzalendo: kushirikiana katika vikundi.
Uhusiano na Masomo mengine: Literacy activities, Religious Activities na
Mathematics Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu siku za wiki.
Uhusiano na Maadili:
heshima kwa siku zilizotengewa shughuli za kidini.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza umuhimu wa shughuli tofauti kwa mfano siku za kwenda shule, siku ya kupumzika na siku ya kwenda maabadini kwa wenzake na miongoni mwa wanajamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyoorodhesha siku za wiki na kuzitungia sentensi
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anaorodhesha siku za wiki kwa haraka na ifaavyo
- anatumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano kwa ubunifu
- anasimulia kisa kwa ufasaha na ubunifu
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anaorodhesha siku za wiki ifaavyo
- anatumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- anasimulia kisa kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa usahihi.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika orodhesha siku za wiki ifaavyo
- ana changamoto katika kutumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- anasimulia baadhi ya visa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto nyingi katika kuorodhesha siku za wiki
- ana changamoto nyingi katika kutumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- Ana changamoto katika kusimulia
visa
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi.