Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua picha za vitu vinavyopatikana shuleni katika kujenga stadi ya kusoma,
  2. kuelezea picha katika hadithi ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
  3. kusikiliza hadithi zikisomwa na  mwalimu kuhusu vitu vinavyopatikana shuleni ili kuimarisha umakinifu,
  4. kusoma hadithi kuhusu shule ili kuimarisha stadi ya kusoma, 
  5. kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa katika kupata mafunzo yanayodhamiriwa,
  6. kuchangamkia kusoma hadithi kuhusu shule.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi kisha asome pamoja na mwalimu na baadaye asome peke yake kwa sauti.
  • Wanafunzi wasomeane hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwenye vifaa vya kiteknolojia k.v. tarakilishi na kinasasauti na kufuatilia yanayosomwa kwenye projekta.
  • Mwanafunzi aweza  kusoma hadithi kutoka kwa jitabu mbele ya darasa. 
  • Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali yanayotokana na hadithi aliyosoma na kusomewa.
  • Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.

MASWALI DADISI

  1. Unaona nini katika picha?
  2. Ni nini kitakachotende-ka katika hadithi?
  3. Ni nani wahusika katika hadithi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza kujiamini/kujithamini –  kuigiza na kusimulia.

Uhusiano na masuala mtambuko na maadili: 

uraia – utangamano wa kijamii  wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.   

Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages Activities  na Environmental activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na mashairi kuhusu shule.

 Uhusiano na Maadili:  

Uwajibikaji.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa shule.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuuliza maswali kuhusu shuleni  
  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia –ako na -enu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini  

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ukakamavu na ufasaha
  • anatumia msamiati wa shuleni katika sentensi ifaavyo na kwa ubunifu
  • anasoma kwa ufasaha
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini kwa ubunifu katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
  • anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anatumia msamiati wa shuleni ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini ifaavyo katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

 . 

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa shuleni katika sentensi
  • ana changamoto kiasi katika kusoma
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • ana changamoto katika kutumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa 
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa shuleni kwenye sentensi
  • ana changamoto nyingi katika kusoma
  • ana changamoto katika kutumia majina ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi 
  • ana changamoto katika kutumia ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo

ana changamoto katika kuandika.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *