Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutamka sauti nne za herufi moja katika kuimarisha stadi ya

kuzungumza,  

  • kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,  
  • kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma, 
  • kusoma herufi za sauti moja kwa ufasaha ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  • kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa kwa ufasaha ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  • kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  • kuandika herufi zinazowakilishwa na sauti lengwa ili kuimarisha stadi ya kuandika,
  • kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa katika mawasiliano ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

Mwanafunzi aweza kutambua sauti /p/, /f/ na /v/ katika maneno.

  • Mwanafunzi asikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha atamke pamoja na mwalimu na

mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili na kama darasa.

  • Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno.
  • Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kusikiliza matamshi ya sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi.
  • Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno.
  • Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
  • Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kwa kugawa maneno marefu katika sehemu ndogo ndogo.
  • Mwanafunzi aweza  kufinyanga maumbo ya herufi.
  • Mwanafunzi aandike herufi za  sauti alizosoma hewani na vitabuni.
  • Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa wakiwa wawili wawili. 
  • Mwanafunzi aweza kutumia  vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta na kipasasauti kusikiliza na kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
  • Mwanafunzi aandike maumbo ya herufi na maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa.
  • Mwanafunzi asikilize imla inayojumuisha maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na kuyaandika.

MASWALI DADISI

1) Ni sauti zipi unazojua kutamka?

  • Unajua kusoma herufi na maneno gani?
  • Unajua kuandika herufi na maneno gani?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika shughuli za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko:  uraia – haki za watoto -wanafunzi wanahamasishwa kuhusu haki zake.                   

Uhusiano na Masomo mengine: Environmental Activities

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na mashairi kuhusu haki za watoto.

 Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji haki za kijamii heshima.

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu haki za watoto.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuuliza maswali kuhusu haki za watoto 
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
  • kuchunguza jinsi anavyotumia vizuri na vibaya katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

 Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema na kwa ukakamavu
  • anatambua haki za watoto na kuzitilia maanani katika mawasiliano 
  • anatumia msamiati wa haki za watoto kwa ubunifu katika sentensi
  • anasoma kwa ufasaha
  • anatetea haki za watoto kwa ukakamavu
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo na kwa ubunifu wa hali ya juu.
  • anaandika kwa hati nadhifu.

 Kufikia Matarajio

  • Mwanafunzi,
  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anatambua haki za watoto 
  • anatumia msamiati wa haki za watoto ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anatetea haki za watoto
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo anaandika kwa hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • anatambua haki za watoto 
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
  • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • ana changamoto  kiasi katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

  • Mwanafunzi,
  • ana changamoto katika  kutamka sauti lengwa
  • ana changamoto katika kutambua haki za watoto 
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kusoma kazi anazopewa
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu kwenye  hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • ana changamoto katika kutumia  vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
  • ana changamoto katika kusoma.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *