Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua picha za watu na kazi mbalimbali ili kuimarisha ufahamu wa hadithi,
  2. kusikiliza hadithi ikisomwa na mwalimu kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha usomaji na usikivu,
  3. kusoma hadithi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  4. kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu kazi mbalimbali  ili kupata ujumbe,
  5. kuchangamkia kusoma hadithi.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
  • Wanafunzi waweza kusoma katika darasa, wakiwa wawili na baadaye mwanafunzi asome peke yake.
  • Mwanafunzi anaweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi na projekta.
  • Mwanafunzi aweza  kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa. 
  • Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma.

MASWALI DADISI

  1. Unaona nini kwenye picha?
  2. Ni aina gani ya kazi ambayo imewasilishwa kwenye picha?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana kufanya kazi katika vikundi

kujiamini/kujithamini – kuthamini na kutambua kazi mbalimbali; Kujibu maswali ya kisarufi vilivyo ubunifu – Katika utunzi wa sentensi na kujibu maswali ya ufahamu ambayo majibu yake si ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

shughuli zinazomsaidia mwanafunzi: mwongozo wa ajira – kuthamini kazi mbalimbali

Uhusiano na masomo mengine: Engilish Activities na Environmental Activities

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji; uzalendo; umoja na heshima

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia wazazi katika kazi za nyumbani na katika jamii kuthamini kazi zinazofanywa na wazazi, ndugu na watu wengine katika jamii.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo yanayohusu kazi mbalimbali kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu kazi mbalimbali katika tamasha za muziki

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotambua kazi mbalimbali 
  • kuchunguza anavyotumia ukanusho wa nyakati katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyosoma na kusimulia hadithi 
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
  • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali kwa ufasaha.
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia kikomo ipasavyo
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo.
  • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali 
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha 
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia kikomo ipasavyo
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anataja kazi mbalimbali
  • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi  vilivyo
  • anafahamu baadhi ya hadithi alizosoma au kusomewa.
  • anatumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti 
  • ana changamoto katika kuelezea kazi mbalimbali
  • ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi 
  • anachangamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa 
  • ana changamoto katika kutumia kikomo 

ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyopewa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *