Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua msamiati unaohusiana na shughuli za sokoni ili kuimarisha mawasiliano,
 2. kusoma msamiati wa sokoni ili kujenga usomaji bora,  
 3. kufahamu maana ya msamiati unaotumiwa sokoni ili kuwezesha mawasiliano,
 4. kutunga sentensi akitumia msamiati wa sokoni ili kuimarisha mawasiliano,
 5. kuandika maneno na sentensi akitumia msamiati wa sokoni ili kuimarisha stadi ya kuandika,
 6. kuthamini shughuli za sokoni. 

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

 • Mwanafunzi asome maneno  kuhusu soko kwenye kadi na chati.
 • Mwanafunzi afafanue  maana ya  msamiati wa sokoni k.v mkokoteni, vibanda, ratili, bidhaa, risiti, dalali, mnunuzi, muuzaji na  mchuuzi).
 • Mwanafunzi achore vitu vipatikanavyo sokoni.
 • Mwanafunzi aweza kutazama picha au video za vitu vya sokoni zikiambatanishwa na sauti na maneno.
 • Mwanafunzi aambatanishe majina na vitu vipatikanavyo sokoni.
 • Mwanafunzi aweza  kujaza nafasi katika sentensi kwa maneno yanayotumiwa sokoni.
 • Mwanafunzi anakili msamiati kuhusu shughuli za sokoni.
 • Mwanafunzi atunge sentensi akitumia msamiati kuhusu shughuli za sokoni.

MASWALI DADISI

 1. Ni msamiati upi unaotumika sokoni?
 2. Je, unaweza kuchora bidhaa gani zinazopatikana sokoni?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendeleza ujifunzaji – kusoma hadithi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya masuala ya kifedha – kujadili umuhimu wa sokoni.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kushiriki katika kuigiza shughuli za sokoni.

Uhusiano na Maadili: 

uadilifu katika shughuli za sokoni umoja – Hamna biashara inayoweza kunawiri pasipo na umoja heshima ni muhimu popote watu wanapoingiliana hasa sokoni uwajibikaji – Mwenye biashara na mnunuzi sharti wawajibike katika shughuli husika.

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia jamii katika shughuli zinazohusu soko.

Mapendekezo ya Tathmini:

• kuchunguza anavyotumia msamiati wa sokoni katika mawasiliano 

 • kuchunguza anavyotumia ndani ya na nje ya katika mawasiliano
 • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
 • kufuatilia mwandiko wake.
 •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatambua na kutumia msamiati unaotumika sokoni
 • anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ubunifu na ukakamavu
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni kwa ufasaha
 • anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi zenye ubunifu wa hali ya juu
 • anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatambua msamiati unaotumika sokoni
 • anasimulia visa kuhusu sokoni kwa ukakamavu
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
 • anatumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
 • anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatambua baadhi ya msamiati unaotumika sokoni
 • anasimulia baadhi ya visa kuhusu sokoni
 • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
 • ana changamoto kiasi katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
 • anaandika kisa kinachohusiana na sokoni kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutambua msamiati unaotumika sokoni
 • ana changamoto katika kusimulia visa kuhusu sokoni
 • ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu sokoni
 • ana changamoto katika kutumia ndani ya na nje ya kutunga sentensi sahihi
 • ana changamoto katika kuandika kisa kinachohusiana na sokoni.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *