SARUFI
Ni utaratibu wa sheria zinazotawala matumizi sahihi ya muundo wa lugha.sheria hizi za lugha ndizo huleta ufasaha na usanifu katika luhga na kumwezesha mzungumzaji kuelewa tungo zinazotolewa na mzungumzaji. Kila lugha huwa na sheria zake katika utunzi wa maneno.
AINA ZA MANENO
kuna aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili. Hizi ni
a. vivumishi
b. viwakilishi
c. nomino
d. vielezi
e. vihusishi
f. vihisishi
g. viunganishi
h. vitenzi
NOMINO
Ni aina ya maneno inayotaja majina ya watu, mahali , kitu , au hali. Ili sentensi iwe kamili lazima nomino au kiwakilishi chake kitumiwe. Kuna aina saba za nomino , hizi ni:
Nomino za pekee/ maalum
Hizi ni nomino halisi zinazotaja majina ya watu, mahali, siku au miezi vitu na Mungu
Nomino hizi zinapo andikwa ,hutangulizw kwa herufi kubwa.nomino hizi ni:
Nomino zinazotaja mahali: Kenya, Tanzania , Eldoret Kisumu, Mlima Kenya, Mto Nyiro .n.k
Nomino zinazotaja siku : Jumapil, Jumanne n.k
Nomino zinazotaja sikukuu: Siku ya Madaraka, Krisimasi, Iddi Mubarak n.k Nomino zinazotaja majina ya watu: Faith, Adul, Jelimo, Nafula. Otieno. Nk Nomino zinazotaja miezi: Agosti, January , Oktoba.
Nomino zinazotaja dini: Kiyahudi Kiiislamu , Kikristo.
Nomino zinazotaja luhga na lahaja: Kingereza , Kiamu, Kiarabu Kijaluo.
NOMINO ZA KAWAIDA
Nomino hizi hutaja vitu vya kawaida visivyo vya kipekee, havina ubainifu wowote.sio lazima ziwe na herufi kubwa katika maandishi kama vile zilivyo nomino za pekee.nomino hizi zinaweza kuwa na umoja na wingi, hata hivyo kuna baahdi ya nomino za kawaida ambazo zina umoja au wingi tu.
Kwa mfano:
mwalimu/ walimu
kiti/viti
mtu/watu
redio (haina wingi)
NOMINO ZA DHAHANIA
Ni majina ambayo hufikiriwa tu , hayawezi kugusika , kuonekana, kunusika wala kusikika. Mara nyingi huanza kwa kiambishi ‘U’ ingawa zingine zinaweza kuanza kwa herufi tofauti. Nomino hizi huwa katika fikra au akilini ma mtu.
Kwa mfano : ujinga, wivu , urembo, unono, woga ,wema , chuki mawaidha, utukufu mapenzi.
NOMINO ZA JAMII/ MAKUNDI
Haya ni majina ambayo hutaja vitu vilivyo katika vikundi, ni nomino ambazo ndani yake kuna vitu vingi. Hufumbata maana ya jumuiya ambayo inasifa yakauli moja.
Kwa mfano : Baraza la mawaziri, halaiki ya watoto ,, umati wa watu.
NOMINO ZA KITENZI JINA/ KITENZI
Ni majina ambayo huundwa kutokana na kitenzi. Hutambulishwa na kiambishi ‘KU’
Kwa mfano kucheza , kuimba , kusoma, kuchunguza.
NOMINO ZA WINGI
Ni nomino ambazo hutokea kwa wingi. Nomino hizi ni za kawaida ila tu hutokea kwa wingi pekee.
Kwa mfano:marashi, matata, marashi , mate , maji , machozi, matumizi, maringo,maudhui.
NOMINO AMBATA/AMBATANI.
Ni majina ambayo huundwa kutokana na maneno mawili mbalimabli Kwa mfano :
mpiga+ picha= mpigapicha
kinasa+sauti= kinasa sauti.
VIVUMISHI
Ni neon linalo eleza zaidi kuhusu nomino huvumisha nomino au majina. Kuna aina mbali mbali za vivumishi
VYA SIFA : ni vivumishi vinavyoeleza sifa za nomino, jinsi gani illivyo. Vivumishi hivi hubadilika kutegemea ngeli za majina, yaani huchukuwa upatanisho wa kisarufi. K.m
-zuri( dada mzuri, ndizi nzuri)
-baya( mtu mbaya, kitu kibaya)
-tamu( chakula kitamu, maneno matamu)
VYA IDADI : vivumishi hivi hufafanua jumla ya vitu vinavyohesabika au visivyohesabika. Vivumishi hivi huchukuwa viambishi kutegemea ngeli inayo husika.
Kwa mfano:
–ili ( watu wawili, mawe mawili, runinga mbili)
-haba( miti haba, watu haba , runinga haba)
-chache( miti michache, watu wachache, , runinga chache)
-ingi( watu wengi, miti nyingi, runinga nyingi)
VIVUMISHI VIONYESHI/ VIASHIRAI
Huonyesha umbali au ukaribu wa nomino. Vivumishi hivi ni kama huyu, hawa, wale, hao, hivi . hapa .pale, mle.
Vivumishi vionyeshi visisitizi
Hutilia mkazo swala , jambo , nomino au jambo Fulani linalorejelewa kwa mfano: pale pale, kukohuko, mumo mumo, uu huu uo huo, uleule.
Vivumishi vya pekee
Vivumishi hivihuchukuwaa viambishi vya ngeli husika.
-enye : hutumika kuonyesha kuwa nomino Fulani inamiliki kitu Fulani k.m
mawe yenye rangi,
watu wenye miraba minne.
-enyewe: husisitiza nomino inayorejelewa.
Kwa mafano
mtoto mwenyewe alienda,
kiti chenyewe kilivunjika.
-ote : huonyesha ujumla wa vitu, watu au kitu pasipo na kubakisha. Kwa mfano wageni wote wamewasili,
mawe yote yali tumika.
0-0te : huonyesha dhna ya bila ubaguzi’. Hutumiwa kumaanisha kila’ Kwa mfano : wageni wowote watawasili.
Mawe yoyote yatatumika
-ingine: hurejelea hali ya kuwa ‘ tofauti au ‘zaidi ya kitu ‘au mahali fulani. Kwa mfano :
Amenunua lori lingine
Kuchapa kwingine kunatisha.
-ingineo: hutumiwa kumaanisha badala ya[ au tofauti na’ kitu kingine. Pia hutumika kama hitimisho ya orodha ambayo haikukamilika.
Kwa mfano:
Watu wengineo hapa ni wabaya
Bakuli linginelo nila mtoto.
VIVUMISHI VIMILIKISHI
Vivumishi hivi huonyesha kitu Fulani kinamilikiwa na nomino fulani. Kwa mfano
Kiti chake
Redio yangu.
Vivumishi hivi hubadilika kiumbo kutegemea ngeli za nomino zinazotumika.
VIVUMISHI VIULIZI
Huuliza swali kuhusiana na nomino inayohusika.
Kwa mfano : kiuulizi gani hakichukui kiambishi chochote na hutumika katika nominoya ngeli zote.
Kiulizi –pi huambishwa kiambishi kwenye nomina ya ngeli.
Kiulizi –ngapi vile vile huambishwa kiambishi lakini huuliza idadi ya nomino katika wingi pekee
vivumishi nomino/ vivumishi vya jina kwa jina.
Hivi ni vivumishi vinavyo tumia nomino au majina kuvumisha nomino nyingine. Huchukuwa nafasi ya kivumishi katika sentensi ambapo huvumisha nomino nyingine.
Kwa mfano
Dada askari aligombea kiti cha eneo bunge.
Mwanasiasa zeruzeru anazifa nzuri.
Vivumishi vya a- unganifu: vivumishi hivi huundwa kwa mzizi wa kihusishi-a unganifu’. Vivumishi hivi hufananua daraja , umilikaji, au aina ya nomino husika. A, unganifu ina nafasi mbalilmbali katika sentensi kutegemea jinsi imetumika.
Kwa mfano
Mtoto wa dada amewasili— umilikaji
Gaidi wa alshabab ni yule – kitambulizi/ aina.
Vivumishi rejeshi ni vivumishi vinavyo onyesha urejelezi wa nomino. Matumizi ya –ye na- o- ya urejeshi.
Kwa mfano
Mbuzi waliokufa watatupwa.
Gaidi aliyeshikwa atashtakiwa.
VITENZI (T)
Ni viarifa au maneno yanayotumiwa kuonyesha vitendo vinavyofanywa.vitenzi huwa na maana mbalimbali kulingana mnyambuliko wake. Kuna ina mbalimbali za vitenzi
VITENZI HALISI
Vi vitenzi vinavyo elezea matukio yanayofanyika, yatakayofanyika, yaliyofanyika, yatakayofanyika kwa nomino au jina k.m kulia kucheza kuimba. Vitenzi halisi vinaweza kutumiwa zaidi ya moja katika sentensi.
Kwa mfano
Rais amewasili nchini.
Mama anawalisha mifugo wake.
Vitenzi vikuu
Ni aina ya vitenzi halisi. Huwa na ujumbe mkuu katika sentensi . Hutokea cha pili katika sentensi iwapo kuna vitenzi viwili katika sentensi.
kwa mfano
Askari wa jiji walikuwa wakiwachapa wachuuzi kiholela
VITENZI VISAIDIZI TS
Hutumika na vitenzi vikuu au halisi katika sentensi ilikukamilisha jambo. Hutokea cha kwanza katika sentensi na kufuatwa na kitenzi halisi au kikuu , ilikuonyesha wakati kama ujao, uliopita ambapo kitendo kimefanyika.
Kwa mfano
Wanamichezo watakuwa wakipewa fidia na serikali.
Mtoto alikuwa akicheza na paka.
VITENZI SAMBAMBA
Ni vitenzi vinavyotokea kwa pamoja katika sentensi ilikutoa ujumbee kamili. Vitenzi vikuu vikitoke pamoja na vitenzi visaidizi kwa mfulilizo basi huitwa vitenzi sambamba.
Kwa mfano
Mtoto alikuwa akicheza na paka.
Baba alikwisha tambua alikuwa mkaidi.
VITENZI VISHIRIKISHI (S)
Ni vitenzi vinavyohitaji vijalizo ilikukamilisha uarifa wao kimaana.vitenzi hivi huonyesha hali au tabia Fulani ya kitu au mtu isiyokuwepo. Vitenzi hivi huwa vya aina mbili
vishikishi vikamilifu
Huchukuwa viambishi vinavyowakilisha nafsi, ngeli, wakati, au hali timilifu k.m ‘ngali’’ kuwa’
Mifano
Mtama ule ungali nkwenye jua.
Wanafunzi wamekuwa na mitihani wiki hii.
VITENZI VISHIRIKISHI VIPUNGUFU
Vitenzi vya aina hii havichukui viambishi vya wakati au ujao, hata hivyo huchukuwa viambishi vya nafsi au nafsi. Hivi ni ni, si ndi-, u, na li
Mifano katika sentensi
Kaka yu mtanashati.
Yeye ni mefu
VIWAKILISHI.
Ni maneno yanayowakilisha nomino katika miktadha mbali mbali. Hufanya kazi ya jina katika sentensi , pia huitw vibadala .kuna aina mbalimbali ya viwakilishi.
VIWAKILISHI NAFSI HURU
Ni vile vinavyotumiwa kuonyesha umoja nawingi wa nafsi tatu za viumbe hai katika ngeli ya A-WA
Mimi , wewe ,sisi, yeye,wao, nyinyi.
17
VIWAKISHI NAFSI TEGEMEZI
Ni viambishi ngeli vya A-WA vinavyoambatanishwa na vitenzi, huwakilisha nafsi ya tatu. K.m
Wa watimba, mimi nitaimba.
VIWAKILISHI VIMILIKISHI
Huonyesha umilikaji wa nomino.
Mifano
Wangu ameenda
Wetu amewasili
VIWAKILISHI VIULIZI
Haya ni maswali yanayo wakilisha nomino.
Kwa mfano
Nani amefariki?
Wapi ni pake?
Ni yupi aliye na dosari?
Viwakilishi vya idadi
Hutaja idadi ya nomino.
Mifano
Wengi wameenda
Mmoja ni wake.
Wachache wataadhibiwa.
18
VIWALKISHI VIONYESHI
Husimamia nomino kuonyesha umbali au ukaribu uliko baina ya vitu viwili au zaidi.
Mifano
Yule ni mamake
Haya yatajadiliwa
Huo unatisha.
VIWAKILISHI VISISITIZI.
Mifano wawahawa ndio wezi waliotuingilia
Kilekile kimevunjika.
VIWAKILISHI VYA ‘A’ UNGANIFU
Huundwa kwa matumizi ya kihusishi -a- unganifu ilimkusimamia nomino. Mifano.
Wa sita amewasili( wakimbiaji)
Wa shamba( jogoo)
VIWAKILISHI VYA SIFA
Viwakilishi hivi huwakilisha tabia ya nomino .
Mifano
Mbaya aliuwawa( mzee)
Mrembo alitekwa nyara( binti)
19
VIWAKILISHI VIREJESHI
Hutokea pale ambapo amba- inasimama badala ya nomino
Mifano
Ambaye ameaga( fidel)
Ambayo haipendezi( chai)
VIWAKILISHI VYA PEKEE
Huchukuwa maumbo mbalimbali kutegemea jinsi inavyotumika. Kwa mfano -ote ( wote) wote waenda
-enye ( mwenye) mwenye kuiba ni Yule)
o-te( zenyewe) zenyewe zmeoza.
-ingine(jingine) jingine ndilo hillo.
-ingineo ( mengineo) mengineo yataliwa
VIUNGANISI ( U)
Ni neno au vifungu vya maneno vinavyo unganisha sentensi, virai au vishazi pamoja. Baadhi ya viunganishi ni kama na, au, lakini, kwa sababu, fauka ya , klicha ya, seuze ya, kwa maana n.k wanafunz i wataje baadhi.
Mifano
Licha ya Musa kuwa mwezi pia ni jambazi.
VIHUSISHI
Ni maneno yanayoonyesha uhusiano uliopo baina ya vitu, mahali watu au neon moja na jingine.
Vihusishi vya wakati kabla ya , tangu, hadi, baadaya.
Vihusishi vya mahali ndani ya , kando ya, chini ya, kati ya, ukingoni vihusishi mwa sababu kwa ajili ya, kwa vile kwa sababu ya n.k
VIHISISHI( H.)
ni maneno yanayo onyesha hisia za mzungumzaji.
Mifano Laiti! Lo! Oyee! Hoyee!
Zoezi
Tunga sentensi kwa kutumia vihisishi vifuatavyo
Maskini!, alhamdulullaih!, bu!, chubwi!
Kiswahili CBC Grade 8 Notes (JSS)
VIELEZI(E)
Ni maneno yanayotoa taarifa zaidi kuhusu kitenzi. Heleza jinsi kitendo kilivyo tendwa tendeka. Kuna aina mbalimbali ya vielezi
VIELEZI VYA NAMNA/JINSI
Hueleza namna au jinsi tendo lilitendeka . tendo lilitendeka aje. Mifano
Mkongwe alitembea poleole.
VIELEZI VYA MAHALI
Huonyesha au kueleza mahali tendo limetoka. Hueza jengwa kwa viambishi tamati –ni mifano alienda nyumbani, au kwa viambishi kama –po, -mo,-ko.
Mifano
Walimoingia wamejaa kunguru
Alikoenda nikucha
VIELEZI VYA WAKATI
hueleza wakati tendo linapofanyika. Huwa maneno kamili ya wakati usiku, jioni au vikadokezwa kwa kiambishi –po kilichoambishwa kwenye wa kitenzi.
Mifano
Alipowasili shimanzi ijijaa.
Tutahudhuria siku ya pili.
Alijifungua usiku.
VIELEZI VYAA IDADI
Hutaja kiasi ambacho kitendo kilifanywa, kitafanywa , huonyesha kitendo kimetendwa mara ngapi kwa mfano mara nyingi, tena, kila mwaka.
MNYAMBULIKO WA VITENZI.
Ni hali ya kuongeza viambishi kwenye mzizi , haswa viambishi tamati na hivyo kukipa kitenzi kinacho husika maana tofauti. Kuna kauli mbalimbali za mnyambuliko
Mfano
Kauli ya kutenda
Huonyesha hali ya kutenda jambo., ambapo kiambishi ‘ a’ huongezwa kwenye mzizi .
Kwa mfano
Lima lima
Soma soma
Kauli ya kutendea
Vitenzi vinavyoishia irabu – ‘ea’
Mifano
Chora chorea
Sema semea
Vitenzi vinavyoishia irabu ‘ – i a’
Mifano
Finya finyia
Sifu sifia
Vitenzi vinavyoishia kwa –lea
Mifano
Ondoa ondolea
Bomoa bomolea
Vitenzi vinavyoishia kwa- lia
Pakua pakuwa
Fua fulia
Kaulika ya kutendwa
Kauli hii huonyesha athari kwa kitu kingine kwamba kitu Fulani kinapokea tendo fulani. Huwa na viambishi tamati au vimbishi hivi
Vinavyoishia kwa – wa
Mifano
Lipa lipwa
Kula kulwa
Vinavyoishia kwa – liwa au lewa
Mifano
Bomoa bomolewa
Chukuwa chukuliwa
Kauli ya kutendeka
Kauli hii huonyesha kutokea kwa jambo bila mhusika
Vitenzi vinavyoishia kwa vokali mbili –‘aa; ua; ia huambishwa -‘lika Mifano
Vaa valika
Tia tilika
Vitenzi vinavyo na irabu ‘i u a’ huchukuwa –‘ika’
Mifano
Fahamu fahamika
pika pikika
Vitenzi vyenye vokali –e, o katika mzizi huishia kwa –eka
Mifano
Osha osheka
Cheza chezeka
Kauli ya kutendua
Huonyesha hali yakinyume, viambishi ni –‘ua , oa.
Mifano
Kunja kunjua
Choma chomoa
Kauli ya kutendana
Ni hali ya kumtendea mtu jambo naye pia anakutendea, kitendo kinaenda pande mbili . kiambishi tamati ni –an’
Mifano
Soma someana
Tega tegeana
Kauli ya kutendata
Huashiriwa kwautumia kiambishi tamati –at’ si maneno yote yanayoweza kunyambulika katika sehemu hii, kunabaadhi tu yameneno yanayoweza kunyambuliwa.
Mifano
Paka pakata
Fumba fumbata
Okoa okota
Kauli ya kutendama
Huonyesha kuwa kitenzi au kitendo kuwa katika hali Fulani bila kubadilika. Vitenzi vya aina hii havipatika kwa urahisi
Mifano
Lala lalama
Kwaa kwama
Ficha fichama
Kauli ya kutendesh
Mnyambuliko huu huchukuwa miundo tofauti tofauti.
Mifano
-esha
Cheza chezesha
Kishio –‘za’
Tembea tembeza
Kishio-vya
Mlevya,
Kishio –‘fya
Ogofya
Kishio –sha
Pikisha
TANABAHI
Sio vitenzi vyote vya lugha ya Kiswahili huwa na sifa ambazo tumeziona hapo juu kunavitenzi vyenye asili ya kigeni na vyenye silabi moja. Katika kunyambua vitenzi vyenye silabi moja huambishwa ‘KU mwanzoni iliviweze kueleweka.
Mfano kula , kupa, kunywa.
Katika Kiswahili kuna wakati ambapo muundo wa neno unaelekea kukubali hali fulani lakini semantiki inakataa.
Kwa mfano
Kuja jiana , jiwa
mfano katika sentensi
mama alijiwa na mumewe.
Kunatofauti kubwa kati ya vitenzivya asili ya kigeni na vitenzi vya asili ya kibantu ambavyo huishia kwa irabu ‘ a’ na vya kigeni kwa u ,e , i.
ZOEZI
Nyambua vitenzi hivi katika kauli ya kutendeana, tendea, tendwa na tendeka. Hesabu
Sadiki
Hasidi
Hujumu
Hoji
Starehe
adhimu
UKANUSHAJI
Ni hali ya kubadilisha usemi Maneno au jambo kutoka hali yakinifu hadi hali ya kukana.
Ukanushaji wa nyakati na hali mbalimbali hutokea kama inavyofuata Wakati uliopo(-li)
sentensi | ukanushaji |
Alicheza jana | hakucheza jana. |
walienda | hawakuenda |
Wakati ulipo(-na)
sentensi | ukanushaji |
Ninasoma | sisomi |
Unapika | Hupiki |
Anacheza | hachezi |
wakati ujao(-ta)
sentensi | ukanushaji |
Kitatupwa hicho | Hakitatupwa hicho |
Ataenda dukani | Hataenda dukani |
Embe litaoza | Embe halitaoza |
HALI
Hali timilifu (me)
Hurejelea matendo yaliotendeka muda mfupi uliopita.
Sentensi | Ukanushaji |
Alshababu wamefika kenya | Alshababu hawajafika Kenya |
Waziri ametoa taarifa kuhusu ushambulizi | Waziri hajatoa taarifa kuhusu shabuliz |
Hali ya mazoea( hu)
Ni matukio yanayofanywa kila mara au mara kwa mara
Sentensi | Ukanushaji |
Mgaganga hugangua | Mganga hagangi |
Wanamgambo hutatiza watu | Wanamgambo hawatatizi watu |
Hali ya (ka)
Hutumika katika vitenzi katika nyakati mbalimbali ujao, uliopita, uliopo, pia huweza kuonyesha matukio yaliyofuatana yalipotokea.
Sentensi | Ukanushaji |
Aliosha nguo akavaa, akaenda kutembea | Hakuosha nguo, hakuvaa wala hakuenda kutembea |
Hali ya (ki)
Hufafanua matukio yalivyotokea yakifuatana au matukio fulani yalitegemea kwa kutokea kwao, hutumiwa kuonyesha masharti
Sentensi | Ukanushaji |
Ukicheza utachafuka | Usipo cheza hutachafuka |
Hali ya- nge, -ngeli, na ngali
Hudhihirisha masharti yasiyowezakana na yanyotegemeana ambapo yale matukio ya baadaye hutegemea ya hapo awali. –nge hudhihirisha uwezokano wa kutokea kwa jambo, – ngeli na – ngali huonyesha kutowezakana kwa jambo.
Sentensi | Ukanushaji |
Ningelipwa ningemsaidia | Nisingelipwa nisingemsaidia |
Angeliitwa ningeliitika | Nisingeli itwa nisingeliitika |
Ungalisikiliza ungalipata Baraka | Usingalisikiza usingalipata Baraka |
Ni nini tofauti ya kinyume na kukanusha?
KINYUME
Ni hali ya kupinga kwa mawazo , jambo au maana husika.
Hali ya vinyume hujidhihirisha katika kategoria tofauti tofauti kwa mfano Vinyume vya vivumishi
-baya -zuri
-fupi -refu
-eupe -eusi
Vivyume vya nomino
Mjinga mwerevu
Njaa shibe
Laana Baraka
Kitwana mjakazi
Vinyume vya vitenzi
Vinyume vya hali ya kutendua
Tega tegua
Bandika bandua
Ziba zibua
Vinyume vya maneno yanayo kinzana
Simama keti
Tembea kimbia
Toka rudi
Fukuza karibisha.
Kiswahili CBC Grade 8 Notes (JSS)
Zingatia
Iwapo vitenzivimefuatana vitenzi sambamba, basi kitenzi cha kwanza ambacho ni kitenzi kisaidizi ndicho hukanushwa.
Kwa mfano
Mama alikuwa akiwatayarishia watoto chakula
Jawabu; mama hakuwa akiwatayarishia watoto chakula.
Huku ukitoa mifano mwafaka, tofautisha dhana zinazofuata
Vitate
Visawe
Vitawe
Vitate
Ni maneno yanyo karibiana kimatamshi lakini yana maana tofauti sana. Mfano
Anwani –kichwa, maelezo ya sanduku la barua
Anuwai—aina tofauti tofauti
Karibia—kusongea au nusura
Karipia—kuzomea , fokea
Bacha – tundu lililoko ukutani
Pacha—vitu viwili vinavyo fanana ambavyo hutokea kwa pamoja, watoto wanao tokana kwa mimba moja.
Vitawe
Menono yenye maana zaidi ya moja, pia huitwa polisemia.
Kaa—aina ya mnyama wa majini, kuketi kitako , kuni ilioungua.
Chache—haribika kwa chakula au chochote kile,kuwa na hasira, chafuka kwa bahari, ongezeka.
Visawe
Ni maneno yenye maana sawa . Pia huitwa ashibahi.
Pesa, fedha ,njenje, ngwenje,
Mtu, insi, binadamu,mja, mahuluki.
Heshima, nidhamu, adabu,fahari utukufu, taadhima.
Barabara baraste njia kuu.
UAKIFISHAJI
Ni hali inayoshughulikia alama zinazotumiwa kisarufi,huleta maana ipasavyo, kurahisisha usomaji , kuongea na hivyo neon au sentensi kufahamika vyema.
Je, matumizi ya alama za uakifishaji ni zipi?
Nukta/kitone/kituo .
Hutumiwa kuonyesha:
a) Maneno yaliofupishwa. Mfano Dkt. Mhe. S.L,P( sanduku la posta.)
b) Hutumiwa mwisho wa sentensi, kuonyesha hoja imekamilika. c) Mgao wa pesa. Mfano 70.30, ( shilingi sabini nukta na senti thelathini), 3.06( shilingi tatu na senti sita)
d) Hutumika kuandika tarehe, ambapo hutenganisha siku, mwezi na mwaka. Mfano 12.4.2016.
Herufi kubwa H
Hutumika :
a) Mwanzoni mwa sentensi.
b) Baada ya nukta au alama y a mshangao au kiulizio..hii huonyesha kwamba sentensi au maneno yanayfuata baada ya alama hizi hujitegemea hivyo huanza kwa herufi kubwa.
c) Mwanzoni mwa majina au nomino mbalimbali mfano majina ya watu, vyeo kwa kifupi,mahali miezi, siku za juma na sikukuu.
d) Kusisitiza jambo katika sentnsi mfano alitaka kujua CHANZO cha mgomo. e) Kuonyesha anwani ya filamu, THE A HUNDREDS ,kitabu mfano GAMBA LA NYOKA.
f) Hutumika katika ufupisho wa neno au maneno mfano S.L.P, ODM, UNEP. herufi ndogo h
Hutumika katika maandishi isipokuwa pale ambapo sentensi mpya inapoanzaau nomino halisi
Ritifaa/ kibainishi ‘
Hutumika katika uandishi wa ving’ong’o ilikuyatofautisha kimatamshi. Mfano ng’ara, ng’oa
Hutumika kuonyesha kudodoshwa kwa herufi katika neon hasaa katika mashairi. Mfano n’kaenda,’ tawasifu (nitawasifu, tutawasifu, watawasifu) Nukta mkato/koloni/nusu/;
a) Hutumika kutenganisha sentensi ndefu sana . Ambao huonyesha kutua au kipumuo
Nilijiuliza maswali mbalimbali, kuhusu chanzo cha yeye kuachishwa kazi; lakini sikupata jawabu, kwa sabau sikuona kosa katika utendakazi wake.
b) Hutumiwa kuunganisha sentensi mfano subira ; huvuta heri.
Nukta pacha/ nukta mbili/koloni
a. Hutumika kuorodhesha maneno mfano baba alimwambia alete : kalamu, vitabu, chaki na wembe.
b. Hutumiwa kutenganisha saa , dakika na sekunde. Mfano 12: 35:o4
c. Hutumika kuonyesha maneno ya msemaji badala ya kutumia alama za nukuu mfano Nilipokutana naye, nilitaka kujua ni kwanini amepote hivyo; alipenduka na kusema: nilikuwa nimtekwa nyara.
d. Hutumika kutenganisha wahusika katika tamthilia mfano
Mwelusi :naliona janga likija kwa kasi mno
Patu : lipi hilo?
e.Huweza kutanguliza kifungu kirefu ambacho kimenukuliwa kutoka kitabuni
Alama ya mshangao/ kihisishi/alama hisi !
Hutumiwa baada ya viigizi
Mfano tulipoenda kwao tulisikia mlio wa paka miow!
Hutumiwa kwa neon linalo onyesha hisia Fulani au mshangao. Mfano Alas ! A ajali hiyo.
Nukta mbilina nakistari:-
Hutumiwa kudokeza ilikutoa mifano. Kwa mfano
Ukiambiwa uoge:- tafuta sabuni, maji na kitambaa cha kutoa uchafu mwilini.
Mkato/ mkwaju(/)
a. Hutumika badala ya ‘au’ mfano Bi/Bw/Prof.
b. Hutumika katika nambari za kumbukumbu . mfano REF/13/07 c. Hutumikakatika kutenganisha tarehe, mwezi n siku mfano 27/1/2016.
Nukta dukukuku …
Hutumika kuonyesha kuwa neon lililoashwa laweza kuwa la matusi , la aibu . ni njia y kuonyesha adhabu kwa lugha
Utingo Yule alitutusi… nilishangaa sana.
Huonyesha kuwa kuna usemi au menono yaliokatwa kabla ya kukamilika. Alama za kiulizi/ kuuliza.?
Hutumika kuuliza jambo au kutaka jawabu
Mfano mbona unalia?
Hutumika kuonyesha iwapo mtu hana uhakika wa jambo au usemi fulani , hivyo hutumia alama za kiulizi
Mfano E. Kezilahabi au Mlokozi ni mwandishi wa kitabu cha GAMBA LA NYOKA?
mabano ( )au parandesi []
Hutumika kufungia nambari au herufi za orodha. Mfano (a) (ii)
Hutumika katika tamthilia ilikufungia maandishi ya maelekezo ya jukwaani. Mfano
Natalia 🙁 akitembea atembea) siamini ananifanyia haya!
Hutumika kuelezea mambo fulani yasio ya lazima katika sentensi lakini huwa na maana kutegemea na muktadha husika
Alipokuwa akirudi nyumbani ,alikutana na vijana wawili( walikuwa wamshikana mikono) alijifanya hajawaona na kwenda zake.
Alama za usemi au kunukuu(‘’ ‘’)
a. Hutumika katika uandishi wa hotuba hasa mwonzo na mwisho wake. b. Hutumiwa katika usemi hasili ambapo maneno yaliyosemwa hunukuliwa.
Mfano mama alisema, ‘’ nitaenda kwenye karamu kesho ‘’.hutumika badala ya kupiga mstari chini ya neo mfano ‘’uzalendo’’
c. Hutumika wakati neno la lugha tofauti linatumiwa katika lugha tofauti Mfano tuliandaliwa ‘’indumbu’’ tulipoenda eneo la magharibi. d. Hutumiwa usisitiza maneno katika sentensi au kifungu mfano Ukija kwenye karamu hakikisha umevalia ‘’ rinda refu nyeusi’’
Kistari kirefu – na kifupi
i. Huonyesha kwamba neno Fulani limefika mwisho na huendelea katika mstari unaofuata.
ii. Hutumika katika uandishi wa tarehe. 12-6-2016.
iii. Hutumika kuunganisha sentensi mbili ambapo sentensi ya pili huwa ufafanuziwa sentensi ya kwanza.
iv. Mfano Haya maeneo maji hushinda yamepotea kila siku- mifereji ya kupitisha maji yalikuwa yamepasuka.
v. Hutumiwa mwanzoni mwa neno kuonyesha kuwa kunakiambishi ambacho kinahitajika. Mfano -pi? –ngineo, -eusi.
Kipumuo/koma/mkato
Honyesha :
a) Kupumzika kwa muda mfupi wakati wa kusoma.
b) Hutumika katika kutenganisha orodha ya vitu mbalimbali. Mfano alinunua:nyanya,vitunguu, mafuta na mboga.
c) Hutumika katika uandishi wa anwani za barua.
d) Hutenganisha sentensi ambazo zingesababisha matatizo ya kueleweka zikisomwa kwa ujumla. Mfano badala ya mamia, maelfu waliwasili. e) Hutumiwa baada ya baadhi ya vihisishi hasa kuuliza mfano je, ni yeye kweli?
f) Hutumika katika tarakimu mfano 356,678. 120,000,05.
Taja matumizi mengine ya alama za uakifishaji.
Get Complete Notes From Here