Please Limited time Offer!

SARUFI 

Ni utaratibu wa sheria zinazotawala matumizi sahihi ya muundo wa lugha.sheria  hizi za lugha ndizo huleta ufasaha na usanifu katika luhga na kumwezesha  mzungumzaji kuelewa tungo zinazotolewa na mzungumzaji. Kila lugha huwa na  sheria zake katika utunzi wa maneno.

AINA ZA MANENO

kuna aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili. Hizi ni

a. vivumishi

b. viwakilishi

c. nomino

d. vielezi

e. vihusishi

f. vihisishi

g. viunganishi

h. vitenzi

NOMINO

Ni aina ya maneno inayotaja majina ya watu, mahali , kitu , au hali. Ili sentensi iwe  kamili lazima nomino au kiwakilishi chake kitumiwe. Kuna aina saba za nomino ,  hizi ni:

Nomino za pekee/ maalum 

Hizi ni nomino halisi zinazotaja majina ya watu, mahali, siku au miezi vitu na  Mungu

Nomino hizi zinapo andikwa ,hutangulizw kwa herufi kubwa.nomino hizi ni:

Nomino zinazotaja mahali: Kenya, Tanzania , Eldoret Kisumu, Mlima  Kenya, Mto Nyiro .n.k

Nomino zinazotaja siku : Jumapil, Jumanne n.k

Nomino zinazotaja sikukuu: Siku ya Madaraka, Krisimasi, Iddi Mubarak n.k Nomino zinazotaja majina ya watu: Faith, Adul, Jelimo, Nafula. Otieno. Nk Nomino zinazotaja miezi: Agosti, January , Oktoba.

Nomino zinazotaja dini: Kiyahudi Kiiislamu , Kikristo.

Nomino zinazotaja luhga na lahaja: Kingereza , Kiamu, Kiarabu Kijaluo.

NOMINO ZA KAWAIDA

Nomino hizi hutaja vitu vya kawaida visivyo vya kipekee, havina ubainifu  wowote.sio lazima ziwe na herufi kubwa katika maandishi kama vile zilivyo  nomino za pekee.nomino hizi zinaweza kuwa na umoja na wingi, hata hivyo kuna  baahdi ya nomino za kawaida ambazo zina umoja au wingi tu.

Kwa mfano: 

mwalimu/ walimu

kiti/viti

mtu/watu

redio (haina wingi)

NOMINO ZA DHAHANIA

Ni majina ambayo hufikiriwa tu , hayawezi kugusika , kuonekana, kunusika wala  kusikika. Mara nyingi huanza kwa kiambishi ‘U’ ingawa zingine zinaweza kuanza  kwa herufi tofauti. Nomino hizi huwa katika fikra au akilini ma mtu.

Kwa mfano : ujinga, wivu , urembo, unono, woga ,wema , chuki mawaidha,  utukufu mapenzi.

NOMINO ZA JAMII/ MAKUNDI

Haya ni majina ambayo hutaja vitu vilivyo katika vikundi, ni nomino ambazo  ndani yake kuna vitu vingi. Hufumbata maana ya jumuiya ambayo inasifa yakauli  moja. 

Kwa mfano : Baraza la mawaziri, halaiki ya watoto ,, umati wa watu.

NOMINO ZA KITENZI JINA/ KITENZI

Ni majina ambayo huundwa kutokana na kitenzi. Hutambulishwa na kiambishi  ‘KU’

Kwa mfano kucheza , kuimba , kusoma, kuchunguza.

NOMINO ZA WINGI

Ni nomino ambazo hutokea kwa wingi. Nomino hizi ni za kawaida ila tu hutokea  kwa wingi pekee.

Kwa mfano:marashi, matata, marashi , mate , maji , machozi, matumizi,  maringo,maudhui.

NOMINO AMBATA/AMBATANI.

Ni majina ambayo huundwa kutokana na maneno mawili mbalimabli  Kwa mfano : 

mpiga+ picha= mpigapicha

kinasa+sauti= kinasa sauti.

VIVUMISHI

Ni neon linalo eleza zaidi kuhusu nomino huvumisha nomino au majina. Kuna aina  mbali mbali za vivumishi

VYA SIFA : ni vivumishi vinavyoeleza sifa za nomino, jinsi gani illivyo.  Vivumishi hivi hubadilika kutegemea ngeli za majina, yaani huchukuwa  upatanisho wa kisarufi. K.m

-zuri( dada mzuri, ndizi nzuri)

-baya( mtu mbaya, kitu kibaya)

-tamu( chakula kitamu, maneno matamu)

VYA IDADI : vivumishi hivi hufafanua jumla ya vitu vinavyohesabika au  visivyohesabika. Vivumishi hivi huchukuwa viambishi kutegemea ngeli inayo  husika.

Kwa mfano: 

–ili ( watu wawili, mawe mawili, runinga mbili)

-haba( miti haba, watu haba , runinga haba)

-chache( miti michache, watu wachache, , runinga chache)

-ingi( watu wengi, miti nyingi, runinga nyingi)

VIVUMISHI VIONYESHI/ VIASHIRAI

Huonyesha umbali au ukaribu wa nomino. Vivumishi hivi ni kama huyu, hawa,  wale, hao, hivi . hapa .pale, mle.

Vivumishi vionyeshi visisitizi

Hutilia mkazo swala , jambo , nomino au jambo Fulani linalorejelewa kwa mfano:  pale pale, kukohuko, mumo mumo, uu huu uo huo, uleule.

Vivumishi vya pekee

Vivumishi hivihuchukuwaa viambishi vya ngeli husika.

-enye : hutumika kuonyesha kuwa nomino Fulani inamiliki kitu Fulani k.m 

mawe yenye rangi,

watu wenye miraba minne.

-enyewe: husisitiza nomino inayorejelewa.

Kwa mafano 

mtoto mwenyewe alienda, 

kiti chenyewe kilivunjika.

-ote : huonyesha ujumla wa vitu, watu au kitu pasipo na kubakisha. Kwa mfano wageni wote wamewasili, 

mawe yote yali tumika.

0-0te : huonyesha dhna ya bila ubaguzi’. Hutumiwa kumaanisha kila’ Kwa mfano : wageni wowote watawasili.

Mawe yoyote yatatumika

-ingine: hurejelea hali ya kuwa ‘ tofauti au ‘zaidi ya kitu ‘au mahali fulani. Kwa mfano :

Amenunua lori lingine

Kuchapa kwingine kunatisha.

-ingineo: hutumiwa kumaanisha badala ya[ au tofauti na’ kitu kingine. Pia  hutumika kama hitimisho ya orodha ambayo haikukamilika.

Kwa mfano:

Watu wengineo hapa ni wabaya

Bakuli linginelo nila mtoto.

VIVUMISHI VIMILIKISHI

Vivumishi hivi huonyesha kitu Fulani kinamilikiwa na nomino fulani.  Kwa mfano 

Kiti chake

Redio yangu.

Vivumishi hivi hubadilika kiumbo kutegemea ngeli za nomino zinazotumika.

VIVUMISHI VIULIZI

Huuliza swali kuhusiana na nomino inayohusika.

Kwa mfano : kiuulizi gani hakichukui kiambishi chochote na hutumika katika  nominoya ngeli zote.

Kiulizi –pi huambishwa kiambishi kwenye nomina ya ngeli.

Kiulizi –ngapi vile vile huambishwa kiambishi lakini huuliza idadi ya nomino  katika wingi pekee

vivumishi nomino/ vivumishi vya jina kwa jina.

Hivi ni vivumishi vinavyo tumia nomino au majina kuvumisha nomino nyingine.  Huchukuwa nafasi ya kivumishi katika sentensi ambapo huvumisha nomino  nyingine.

Kwa mfano 

Dada askari aligombea kiti cha eneo bunge.

Mwanasiasa zeruzeru anazifa nzuri.

Vivumishi vya a- unganifu: vivumishi hivi huundwa kwa mzizi wa kihusishi-a unganifu’. Vivumishi hivi hufananua daraja , umilikaji, au aina ya nomino husika.  A, unganifu ina nafasi mbalilmbali katika sentensi kutegemea jinsi imetumika.

Kwa mfano 

Mtoto wa dada amewasili— umilikaji

Gaidi wa alshabab ni yule – kitambulizi/ aina.

Vivumishi rejeshi ni vivumishi vinavyo onyesha urejelezi wa nomino. Matumizi  ya –ye na- o- ya urejeshi.

Kwa mfano 

Mbuzi waliokufa watatupwa.

Gaidi aliyeshikwa atashtakiwa.

VITENZI (T)

Ni viarifa au maneno yanayotumiwa kuonyesha vitendo vinavyofanywa.vitenzi  huwa na maana mbalimbali kulingana mnyambuliko wake. Kuna ina mbalimbali  za vitenzi

VITENZI HALISI

Vi vitenzi vinavyo elezea matukio yanayofanyika, yatakayofanyika, yaliyofanyika,  yatakayofanyika kwa nomino au jina k.m kulia kucheza kuimba. Vitenzi halisi  vinaweza kutumiwa zaidi ya moja katika sentensi.

Kwa mfano

Rais amewasili nchini.

Mama anawalisha mifugo wake.

Vitenzi vikuu

Ni aina ya vitenzi halisi. Huwa na ujumbe mkuu katika sentensi . Hutokea  cha pili katika sentensi iwapo kuna vitenzi viwili katika sentensi.

kwa mfano

Askari wa jiji walikuwa wakiwachapa wachuuzi kiholela

VITENZI VISAIDIZI TS

Hutumika na vitenzi vikuu au halisi katika sentensi ilikukamilisha jambo.  Hutokea cha kwanza katika sentensi na kufuatwa na kitenzi halisi au kikuu ,  ilikuonyesha wakati kama ujao, uliopita ambapo kitendo kimefanyika.

Kwa mfano

Wanamichezo watakuwa wakipewa fidia na serikali.

Mtoto alikuwa akicheza na paka.

VITENZI SAMBAMBA

Ni vitenzi vinavyotokea kwa pamoja katika sentensi ilikutoa ujumbee kamili.  Vitenzi vikuu vikitoke pamoja na vitenzi visaidizi kwa mfulilizo basi huitwa  vitenzi sambamba.

Kwa mfano

Mtoto alikuwa akicheza na paka.

Baba alikwisha tambua alikuwa mkaidi.

VITENZI VISHIRIKISHI (S)

Ni vitenzi vinavyohitaji vijalizo ilikukamilisha uarifa wao kimaana.vitenzi hivi  huonyesha hali au tabia Fulani ya kitu au mtu isiyokuwepo. Vitenzi hivi huwa vya  aina mbili 

vishikishi vikamilifu 

Huchukuwa viambishi vinavyowakilisha nafsi, ngeli, wakati, au hali timilifu k.m  ‘ngali’’ kuwa’

Mifano

Mtama ule ungali nkwenye jua.

Wanafunzi wamekuwa na mitihani wiki hii.

VITENZI VISHIRIKISHI VIPUNGUFU

Vitenzi vya aina hii havichukui viambishi vya wakati au ujao, hata hivyo  huchukuwa viambishi vya nafsi au nafsi. Hivi ni ni, si ndi-, u, na li

Mifano katika sentensi

Kaka yu mtanashati.

Yeye ni mefu

VIWAKILISHI.

Ni maneno yanayowakilisha nomino katika miktadha mbali mbali. Hufanya kazi  ya jina katika sentensi , pia huitw vibadala .kuna aina mbalimbali ya viwakilishi.

VIWAKILISHI NAFSI HURU

Ni vile vinavyotumiwa kuonyesha umoja nawingi wa nafsi tatu za viumbe hai  katika ngeli ya A-WA

Mimi , wewe ,sisi, yeye,wao, nyinyi.

17

VIWAKISHI NAFSI TEGEMEZI 

Ni viambishi ngeli vya A-WA vinavyoambatanishwa na vitenzi, huwakilisha  nafsi ya tatu. K.m 

Wa watimba, mimi nitaimba.

VIWAKILISHI VIMILIKISHI

Huonyesha umilikaji wa nomino.

Mifano 

Wangu ameenda

Wetu amewasili

VIWAKILISHI VIULIZI

Haya ni maswali yanayo wakilisha nomino.

Kwa mfano

Nani amefariki?

Wapi ni pake?

Ni yupi aliye na dosari?

Viwakilishi vya idadi

Hutaja idadi ya nomino. 

Mifano

Wengi wameenda

Mmoja ni wake.

Wachache wataadhibiwa.

18

VIWALKISHI VIONYESHI

Husimamia nomino kuonyesha umbali au ukaribu uliko baina ya vitu viwili au  zaidi.

Mifano

Yule ni mamake

Haya yatajadiliwa

Huo unatisha.

VIWAKILISHI VISISITIZI.

Mifano wawahawa ndio wezi waliotuingilia

Kilekile kimevunjika.

VIWAKILISHI VYA ‘A’ UNGANIFU

Huundwa kwa matumizi ya kihusishi -a- unganifu ilimkusimamia nomino.  Mifano. 

Wa sita amewasili( wakimbiaji)

Wa shamba( jogoo)

VIWAKILISHI VYA SIFA

Viwakilishi hivi huwakilisha tabia ya nomino .

Mifano 

Mbaya aliuwawa( mzee)

Mrembo alitekwa nyara( binti)

19

VIWAKILISHI VIREJESHI

Hutokea pale ambapo amba- inasimama badala ya nomino 

Mifano 

Ambaye ameaga( fidel)

Ambayo haipendezi( chai)

VIWAKILISHI VYA PEKEE

Huchukuwa maumbo mbalimbali kutegemea jinsi inavyotumika. Kwa mfano -ote ( wote) wote waenda 

-enye ( mwenye) mwenye kuiba ni Yule)

o-te( zenyewe) zenyewe zmeoza.

-ingine(jingine) jingine ndilo hillo.

-ingineo ( mengineo) mengineo yataliwa

VIUNGANISI ( U)

Ni neno au vifungu vya maneno vinavyo unganisha sentensi, virai au vishazi  pamoja. Baadhi ya viunganishi ni kama na, au, lakini, kwa sababu, fauka ya ,  klicha ya, seuze ya, kwa maana n.k wanafunz i wataje baadhi. 

Mifano

 Licha ya Musa kuwa mwezi pia ni jambazi.

VIHUSISHI

Ni maneno yanayoonyesha uhusiano uliopo baina ya vitu, mahali watu au neon  moja na jingine.

Vihusishi vya wakati kabla ya , tangu, hadi, baadaya.

Vihusishi vya mahali ndani ya , kando ya, chini ya, kati ya, ukingoni vihusishi mwa sababu kwa ajili ya, kwa vile kwa sababu ya n.k

VIHISISHI( H.) 

ni maneno yanayo onyesha hisia za mzungumzaji.

Mifano Laiti! Lo! Oyee! Hoyee!

Zoezi

Tunga sentensi kwa kutumia vihisishi vifuatavyo

Maskini!, alhamdulullaih!, bu!, chubwi!

Kiswahili CBC Grade 8 Notes (JSS)

VIELEZI(E)

Ni maneno yanayotoa taarifa zaidi kuhusu kitenzi. Heleza jinsi kitendo kilivyo  tendwa tendeka. Kuna aina mbalimbali ya vielezi

VIELEZI VYA NAMNA/JINSI

Hueleza namna au jinsi tendo lilitendeka . tendo lilitendeka aje. Mifano 

Mkongwe alitembea poleole. 

VIELEZI VYA MAHALI

Huonyesha au kueleza mahali tendo limetoka. Hueza jengwa kwa viambishi  tamati –ni mifano alienda nyumbani, au kwa viambishi kama –po, -mo,-ko.

Mifano 

Walimoingia wamejaa kunguru

Alikoenda nikucha

VIELEZI VYA WAKATI

hueleza wakati tendo linapofanyika. Huwa maneno kamili ya wakati usiku, jioni  au vikadokezwa kwa kiambishi –po kilichoambishwa kwenye wa kitenzi.

Mifano

Alipowasili shimanzi ijijaa.

Tutahudhuria siku ya pili.

Alijifungua usiku.

VIELEZI VYAA IDADI

Hutaja kiasi ambacho kitendo kilifanywa, kitafanywa , huonyesha kitendo  kimetendwa mara ngapi kwa mfano mara nyingi, tena, kila mwaka.

MNYAMBULIKO WA VITENZI.

Ni hali ya kuongeza viambishi kwenye mzizi , haswa viambishi tamati na hivyo  kukipa kitenzi kinacho husika maana tofauti. Kuna kauli mbalimbali za  mnyambuliko

Mfano 

Kauli ya kutenda

Huonyesha hali ya kutenda jambo., ambapo kiambishi ‘ a’ huongezwa kwenye  mzizi .

Kwa mfano 

Lima lima

Soma soma

Kauli ya kutendea

Vitenzi vinavyoishia irabu – ‘ea’

Mifano

Chora chorea

Sema semea

Vitenzi vinavyoishia irabu ‘ – i a’

Mifano

Finya finyia

Sifu sifia

Vitenzi vinavyoishia kwa –lea

Mifano

Ondoa ondolea

Bomoa bomolea

Vitenzi vinavyoishia kwa- lia

Pakua pakuwa

Fua fulia

Kaulika ya kutendwa

Kauli hii huonyesha athari kwa kitu kingine kwamba kitu Fulani kinapokea tendo  fulani. Huwa na viambishi tamati au vimbishi hivi

Vinavyoishia kwa – wa

Mifano

Lipa lipwa

Kula kulwa

Vinavyoishia kwa – liwa au lewa

Mifano

Bomoa bomolewa

Chukuwa chukuliwa

Kauli ya kutendeka 

Kauli hii huonyesha kutokea kwa jambo bila mhusika

Vitenzi vinavyoishia kwa vokali mbili –‘aa; ua; ia huambishwa -‘lika Mifano

Vaa valika

Tia tilika

Vitenzi vinavyo na irabu ‘i u a’ huchukuwa –‘ika’ 

Mifano

Fahamu fahamika

pika pikika

Vitenzi vyenye vokali –e, o katika mzizi huishia kwa –eka

Mifano

Osha osheka

Cheza chezeka

Kauli ya kutendua

Huonyesha hali yakinyume, viambishi ni –‘ua , oa.

Mifano

Kunja kunjua

Choma chomoa

Kauli ya kutendana

Ni hali ya kumtendea mtu jambo naye pia anakutendea, kitendo kinaenda pande  mbili . kiambishi tamati ni –an’

Mifano 

Soma someana

Tega tegeana

Kauli ya kutendata

Huashiriwa kwautumia kiambishi tamati –at’ si maneno yote yanayoweza  kunyambulika katika sehemu hii, kunabaadhi tu yameneno yanayoweza  kunyambuliwa.

Mifano

Paka pakata

Fumba fumbata

Okoa okota

Kauli ya kutendama

Huonyesha kuwa kitenzi au kitendo kuwa katika hali Fulani bila kubadilika.  Vitenzi vya aina hii havipatika kwa urahisi

Mifano

Lala lalama

Kwaa kwama

Ficha fichama

Kauli ya kutendesh

Mnyambuliko huu huchukuwa miundo tofauti tofauti.

Mifano 

-esha 

Cheza chezesha

Kishio –‘za’

Tembea tembeza

Kishio-vya

Mlevya, 

Kishio –‘fya

Ogofya 

Kishio –sha

Pikisha

TANABAHI

Sio vitenzi vyote vya lugha ya Kiswahili huwa na sifa ambazo tumeziona hapo  juu kunavitenzi vyenye asili ya kigeni na vyenye silabi moja. Katika kunyambua  vitenzi vyenye silabi moja huambishwa ‘KU mwanzoni iliviweze kueleweka.

Mfano kula , kupa, kunywa.

Katika Kiswahili kuna wakati ambapo muundo wa neno unaelekea kukubali hali  fulani lakini semantiki inakataa.

Kwa mfano 

Kuja jiana , jiwa 

 mfano katika sentensi

mama alijiwa na mumewe.

Kunatofauti kubwa kati ya vitenzivya asili ya kigeni na vitenzi vya asili ya  kibantu ambavyo huishia kwa irabu ‘ a’ na vya kigeni kwa u ,e , i.

ZOEZI

Nyambua vitenzi hivi katika kauli ya kutendeana, tendea, tendwa na tendeka. Hesabu

Sadiki

Hasidi

Hujumu

Hoji

Starehe

adhimu

UKANUSHAJI

Ni hali ya kubadilisha usemi Maneno au jambo kutoka hali yakinifu hadi hali ya  kukana.

Ukanushaji wa nyakati na hali mbalimbali hutokea kama inavyofuata Wakati uliopo(-li)

sentensiukanushaji
Alicheza janahakucheza jana.
waliendahawakuenda

Wakati ulipo(-na)

sentensiukanushaji
Ninasomasisomi
UnapikaHupiki
Anachezahachezi

wakati ujao(-ta)

sentensiukanushaji
Kitatupwa hichoHakitatupwa hicho
Ataenda dukaniHataenda dukani
Embe litaozaEmbe halitaoza

HALI

Hali timilifu (me)

Hurejelea matendo yaliotendeka muda mfupi uliopita.

SentensiUkanushaji
Alshababu wamefika kenyaAlshababu hawajafika Kenya
Waziri ametoa taarifa kuhusu  ushambuliziWaziri hajatoa taarifa kuhusu  shabuliz

Hali ya mazoea( hu)

Ni matukio yanayofanywa kila mara au mara kwa mara

SentensiUkanushaji
Mgaganga huganguaMganga hagangi
Wanamgambo hutatiza watuWanamgambo hawatatizi watu

Hali ya (ka)

Hutumika katika vitenzi katika nyakati mbalimbali ujao, uliopita, uliopo, pia  huweza kuonyesha matukio yaliyofuatana yalipotokea.

SentensiUkanushaji
Aliosha nguo akavaa, akaenda  kutembeaHakuosha nguo, hakuvaa wala  hakuenda kutembea

Hali ya (ki)

Hufafanua matukio yalivyotokea yakifuatana au matukio fulani yalitegemea kwa  kutokea kwao, hutumiwa kuonyesha masharti

SentensiUkanushaji
Ukicheza utachafukaUsipo cheza hutachafuka

Hali ya- nge, -ngeli, na ngali

Hudhihirisha masharti yasiyowezakana na yanyotegemeana ambapo yale matukio  ya baadaye hutegemea ya hapo awali. –nge hudhihirisha uwezokano wa kutokea  kwa jambo, – ngeli na – ngali huonyesha kutowezakana kwa jambo.

SentensiUkanushaji
Ningelipwa ningemsaidiaNisingelipwa nisingemsaidia
Angeliitwa ningeliitikaNisingeli itwa nisingeliitika
Ungalisikiliza ungalipata BarakaUsingalisikiza usingalipata Baraka

Ni nini tofauti ya kinyume na kukanusha?

KINYUME

Ni hali ya kupinga kwa mawazo , jambo au maana husika.

Hali ya vinyume hujidhihirisha katika kategoria tofauti tofauti kwa mfano Vinyume vya vivumishi

-baya -zuri

-fupi -refu

-eupe -eusi

Vivyume vya nomino

Mjinga mwerevu

Njaa shibe

Laana Baraka 

Kitwana mjakazi

Vinyume vya vitenzi

Vinyume vya hali ya kutendua

Tega tegua

Bandika bandua

Ziba zibua

Vinyume vya maneno yanayo kinzana

Simama keti

Tembea kimbia

Toka rudi

Fukuza karibisha.

Kiswahili CBC Grade 8 Notes (JSS)

Zingatia 

Iwapo vitenzivimefuatana vitenzi sambamba, basi kitenzi cha kwanza ambacho ni  kitenzi kisaidizi ndicho hukanushwa. 

Kwa mfano

Mama alikuwa akiwatayarishia watoto chakula

Jawabu; mama hakuwa akiwatayarishia watoto chakula.

Huku ukitoa mifano mwafaka, tofautisha dhana zinazofuata

Vitate

Visawe

Vitawe

Vitate

Ni maneno yanyo karibiana kimatamshi lakini yana maana tofauti sana. Mfano

Anwani –kichwa, maelezo ya sanduku la barua

Anuwai—aina tofauti tofauti

Karibia—kusongea au nusura

Karipia—kuzomea , fokea

Bacha – tundu lililoko ukutani

Pacha—vitu viwili vinavyo fanana ambavyo hutokea kwa pamoja, watoto wanao  tokana kwa mimba moja.

Vitawe

Menono yenye maana zaidi ya moja, pia huitwa polisemia.

Kaa—aina ya mnyama wa majini, kuketi kitako , kuni ilioungua.

Chache—haribika kwa chakula au chochote kile,kuwa na hasira, chafuka kwa  bahari, ongezeka.

Visawe

Ni maneno yenye maana sawa . Pia huitwa ashibahi.

Pesa, fedha ,njenje, ngwenje,

Mtu, insi, binadamu,mja, mahuluki.

Heshima, nidhamu, adabu,fahari utukufu, taadhima.

Barabara baraste njia kuu.

UAKIFISHAJI

Ni hali inayoshughulikia alama zinazotumiwa kisarufi,huleta maana ipasavyo,  kurahisisha usomaji , kuongea na hivyo neon au sentensi kufahamika vyema.

Je, matumizi ya alama za uakifishaji ni zipi?

Nukta/kitone/kituo .

Hutumiwa kuonyesha:

a) Maneno yaliofupishwa. Mfano Dkt. Mhe. S.L,P( sanduku la  posta.)

b) Hutumiwa mwisho wa sentensi, kuonyesha hoja imekamilika. c) Mgao wa pesa. Mfano 70.30, ( shilingi sabini nukta na senti  thelathini), 3.06( shilingi tatu na senti sita)

d) Hutumika kuandika tarehe, ambapo hutenganisha siku, mwezi na  mwaka. Mfano 12.4.2016.

Herufi kubwa H

Hutumika :

a) Mwanzoni mwa sentensi.

b) Baada ya nukta au alama y a mshangao au kiulizio..hii huonyesha kwamba  sentensi au maneno yanayfuata baada ya alama hizi hujitegemea hivyo  huanza kwa herufi kubwa.

c) Mwanzoni mwa majina au nomino mbalimbali mfano majina ya watu, vyeo  kwa kifupi,mahali miezi, siku za juma na sikukuu.

d) Kusisitiza jambo katika sentnsi mfano alitaka kujua CHANZO cha mgomo. e) Kuonyesha anwani ya filamu, THE A HUNDREDS ,kitabu mfano  GAMBA LA NYOKA.

f) Hutumika katika ufupisho wa neno au maneno mfano S.L.P, ODM, UNEP. herufi ndogo h

Hutumika katika maandishi isipokuwa pale ambapo sentensi mpya inapoanzaau  nomino halisi

Ritifaa/ kibainishi ‘

Hutumika katika uandishi wa ving’ong’o ilikuyatofautisha kimatamshi.  Mfano ng’ara, ng’oa

Hutumika kuonyesha kudodoshwa kwa herufi katika neon hasaa katika mashairi. Mfano n’kaenda,’ tawasifu (nitawasifu, tutawasifu, watawasifu) Nukta mkato/koloni/nusu/;

a) Hutumika kutenganisha sentensi ndefu sana . Ambao huonyesha kutua au  kipumuo

Nilijiuliza maswali mbalimbali, kuhusu chanzo cha yeye kuachishwa kazi; lakini  sikupata jawabu, kwa sabau sikuona kosa katika utendakazi wake.

b) Hutumiwa kuunganisha sentensi mfano subira ; huvuta heri.

Nukta pacha/ nukta mbili/koloni

a. Hutumika kuorodhesha maneno mfano baba alimwambia alete : kalamu,  vitabu, chaki na wembe.

b. Hutumiwa kutenganisha saa , dakika na sekunde. Mfano 12: 35:o4

c. Hutumika kuonyesha maneno ya msemaji badala ya kutumia alama za nukuu  mfano Nilipokutana naye, nilitaka kujua ni kwanini amepote hivyo;  alipenduka na kusema: nilikuwa nimtekwa nyara.

d. Hutumika kutenganisha wahusika katika tamthilia mfano

 Mwelusi :naliona janga likija kwa kasi mno

 Patu : lipi hilo?

 e.Huweza kutanguliza kifungu kirefu ambacho kimenukuliwa kutoka kitabuni

Alama ya mshangao/ kihisishi/alama hisi !

Hutumiwa baada ya viigizi

Mfano tulipoenda kwao tulisikia mlio wa paka miow!

Hutumiwa kwa neon linalo onyesha hisia Fulani au mshangao. Mfano Alas ! A ajali hiyo.

Nukta mbilina nakistari:-

Hutumiwa kudokeza ilikutoa mifano. Kwa mfano

Ukiambiwa uoge:- tafuta sabuni, maji na kitambaa cha kutoa uchafu mwilini.

Mkato/ mkwaju(/)

a. Hutumika badala ya ‘au’ mfano Bi/Bw/Prof.

b. Hutumika katika nambari za kumbukumbu . mfano REF/13/07 c. Hutumikakatika kutenganisha tarehe, mwezi n siku mfano 27/1/2016.

Nukta dukukuku …

Hutumika kuonyesha kuwa neon lililoashwa laweza kuwa la matusi , la aibu . ni  njia y kuonyesha adhabu kwa lugha

Utingo Yule alitutusi… nilishangaa sana.

Huonyesha kuwa kuna usemi au menono yaliokatwa kabla ya kukamilika. Alama za kiulizi/ kuuliza.?

Hutumika kuuliza jambo au kutaka jawabu

Mfano mbona unalia?

Hutumika kuonyesha iwapo mtu hana uhakika wa jambo au usemi fulani , hivyo  hutumia alama za kiulizi

Mfano E. Kezilahabi au Mlokozi ni mwandishi wa kitabu cha GAMBA LA  NYOKA?

mabano ( )au parandesi []

Hutumika kufungia nambari au herufi za orodha. Mfano (a) (ii)

Hutumika katika tamthilia ilikufungia maandishi ya maelekezo ya jukwaani.  Mfano

Natalia 🙁 akitembea atembea) siamini ananifanyia haya!

Hutumika kuelezea mambo fulani yasio ya lazima katika sentensi lakini huwa na  maana kutegemea na muktadha husika

Alipokuwa akirudi nyumbani ,alikutana na vijana wawili( walikuwa wamshikana  mikono) alijifanya hajawaona na kwenda zake.

Alama za usemi au kunukuu(‘’ ‘’)

a. Hutumika katika uandishi wa hotuba hasa mwonzo na mwisho wake. b. Hutumiwa katika usemi hasili ambapo maneno yaliyosemwa hunukuliwa.

Mfano mama alisema, ‘’ nitaenda kwenye karamu kesho ‘’.hutumika badala ya  kupiga mstari chini ya neo mfano ‘’uzalendo’’

c. Hutumika wakati neno la lugha tofauti linatumiwa katika lugha tofauti Mfano tuliandaliwa ‘’indumbu’’ tulipoenda eneo la magharibi. d. Hutumiwa usisitiza maneno katika sentensi au kifungu mfano Ukija kwenye karamu hakikisha umevalia ‘’ rinda refu nyeusi’’

Kistari kirefu – na kifupi

i. Huonyesha kwamba neno Fulani limefika mwisho na huendelea katika mstari  unaofuata.

ii. Hutumika katika uandishi wa tarehe. 12-6-2016.

iii. Hutumika kuunganisha sentensi mbili ambapo sentensi ya pili huwa  ufafanuziwa sentensi ya kwanza. 

iv. Mfano Haya maeneo maji hushinda yamepotea kila siku- mifereji ya  kupitisha maji yalikuwa yamepasuka.

v. Hutumiwa mwanzoni mwa neno kuonyesha kuwa kunakiambishi ambacho  kinahitajika. Mfano -pi? –ngineo, -eusi.

Kipumuo/koma/mkato

Honyesha :

a) Kupumzika kwa muda mfupi wakati wa kusoma.

b) Hutumika katika kutenganisha orodha ya vitu mbalimbali. Mfano  alinunua:nyanya,vitunguu, mafuta na mboga.

c) Hutumika katika uandishi wa anwani za barua.

d) Hutenganisha sentensi ambazo zingesababisha matatizo ya kueleweka  zikisomwa kwa ujumla. Mfano badala ya mamia, maelfu waliwasili. e) Hutumiwa baada ya baadhi ya vihisishi hasa kuuliza mfano je, ni yeye kweli?

f) Hutumika katika tarakimu mfano 356,678. 120,000,05.

Taja matumizi mengine ya alama za uakifishaji.

Get Complete Notes From Here

Grade 8 Notes CBC Junior Secondary 2024

Download Latest Grade 8 Exams 2024.

Grade 8 exams are available now link to grade 8 exams

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *