Please Limited time Offer!

November 2022 – Muda Saa 1

MASWALI

Swali la 1 hadi la 5.
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

(Babu ameketi chini ya mti akisoma gazeti. Analiweka gazeti kando anapomwona Muli)
Muli: (akimsogelea Babu) Shikamoo Babu?
Babu: (kwa tabasamu) Marahaba mjukuu wangu! Habari za shule?
Muli: Njema babu! (kimya) Babu, nikwambie kitu?
Babu: Naam, niambie mjukuu wangu.
Muli: Wenzangu walinichagua kuwa kiranja wa darasa.
Babu: Hongera! Jambo zuri.
Muli: (akijikuna kichwa) Lakini Babu, sijui ninastahili kufanya nini ili niwe kiongozi bora.
Babu: Aha! Muli, sikiliza, ili kuwa kiongozi bora unastahili kuwa na maadili.
Muli: Ooh! Maadili…
Babu: Naam mjukuu wangu. Unaweza kuonyesha maadili kwa namna mbalimbali. Kwanza uwahudumie wenzako bila kuwabagua.
Muli: Kweli Babu, ninafikiria pia ninastahili kuwaonyesha upendo.
Babu: Ndiyo Muli. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwajali na kuwasaidia wenzako.
Muli: Kweli Babu! Ninaona kwamba heshima, umoja na ushirikiano pia ni mambo muhimu.
Babu: Haswa! Heshima si utumwa. Je, unaweza kuonyesha heshima kwa njia gani?
Muli: (Kwa ujasiri) Kwa kuwaamkua wote na kusikiliza wanayoyasema.
Babu: Vyema! Unastahili pia kuwa mwaminifu. Tunaonyesha uaminifu kwa kusema ukweli na kufanya mambo inavyostahili.
Muli: Asante babu! Hakika umenifunza mengi.

 1. Muli alipoulizwa na babu kuhusu habari za shule, alimjibu
  1. Naam
  2. Njema
  3. Shikamoo
  4. Marahaba
 2. Maneno yafuatayo yametumiwa katika mazungumzo. Lipi halionyeshi adabu?
  1. Karibu
  2. Naam
  3. Asante
  4. Kweli
 3. Ni jibu lipi linaloonyesha maadili ambayo Babu alimfunza Muli?
  1. Kuhudumia, kuheshimu na kusikiliza. 
  2. Kuamkua, kusikiliza na kujali.
  3. Kujali, kusaidia na kuwa mwaminifu.
  4. Kuwa na heshima, kushirikiana na kusaidia.
 4. Unafikiri Muli atafanya nini baada ya kumuaga Babu?
  1. Atafurahia kuwa kiongozi shuleni.
  2. Atazingatia mawaidha ya babu.
  3. Atawaeleza wenzake kuhusu alivyokutana na babu.
  4. Atawapongeza wenzake kwa kumchagua kuwa kiranja
 5. Neno maadili limetumika katika mazungumzo maana yake ni
  1. Mienendo mizuri inayofaa kuzingatiwa na mtu.
  2. Maonyo ambayo hutolewa mtu anapokosea. 
  3. Matendo ambayo mtu huwafanyia wenzake.
  4. Mitindo mipya inayofuatwa na mtu.

Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Sungura alirauka kabla ya jua kuchomoza. Alianza safari ya kwenda kumtembelea shangazi yake. Njiani alipanda milima na kuvuka mabonde. Jua lilipochomoza, aligundua kuwa alikuwa ametembea sana ila hakuwa amefika kwa shangazi yake. Alikuwa anaelekea kusini badala ya kaskazini. Kumbe alikuwa amepotea njia! “Nitafanya nini? Nimepotea njia,” Sungura alijisemea kwa sauti.
“Nitakusaidia,” alisema Kobe aliyekuwa kichakani, hapo karibu.
“Asante sana Kobe. Sikuwa nimekuona. Tafadhali nisaidie.” Sungura alimwomba Kobe.
“Unakwenda upande gani?” Kobe alimuuliza Sungura.
“Naelekea kaskazini, anakoishi shangazi yangu,” Sungura alimjibu Kobe.
“Jua huchomoza upande wa Mashariki wa dira kila asubuhi. Ukitaka kwenda Kaskazini, simama kisha unyooshe mikono yako juu. Mkono wa kulia uuelekeze kunakotoka jua. Huko ndiko Mashariki. Nao mkono wa kushoto uuelekeze upande huo mwingine. Huko ndiko Magharibi,” Kobe alimweleza Sungura huku akimwonyesha kwa vitendo.
“Kwa hivyo uso wangu utakuwa unaangalia Kaskazini huku mgongo wangu ukiwa upande wa Kusini” Sungura alisema kwa furaha.
“Wewe ni mwanafunzi mzuri. Unaelewa haraka. Umelenga ndipo,” Kobe alimwambia Sungura kwa bashasha.
“Undugu ni kufaana. Asante sana Kobe,”
Sungura aligeuka akarudi hadi kwake ili kuanza safari upya.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

One thought on “Kiswahili-Grade 6 KPSEA 2022 Past Papers Questions and Answers”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *