MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua matumizi ya –angu na –etu katika mawasiliano,
- kutumia –angu na – etu katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano,
- kufurahia kutumia –angu na – etu katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atunge sentensi zenye matumizi ya angu na –etu.
- Mwanafunzi aandike sentensi zenye kuhusisha –angu na –etu.
- Mwanafunzi asome sentensi zenye kutumia maneno angu na –etu.
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia angu na –etu.
- Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la kujaza mapengo kwa tarakilishi (mchezo wa kuvuta na kutia kapuni).
MASWALI DADISI
- Je, ni maneno gani tunayotumia
- kuonyesha kuwa kitu ni chako au ni chenu?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
- mawasiliano na ushirikiano – kujadili katika makundi au wawili wawili
- hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kujua vyakula zaidi
- ujuzi wa kidijitali –matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya afya: magonjwa yanayohusiana na vyakula – kuthamini vyakula vya kiasili.
Uhusiano na Masomo mengine:
Health and Nutrition Activities na Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
nyimbo na Mashairi kuhusu vyakula vya kiasili
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu vyakula vya kiasili
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia –angu na -etu katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anaelezea mifano ya vyakula vya
kiasili
- anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja mifano ya vyakula vya
kiasili
- anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anataja mifano ya vyakula vya
kiasili
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kusoma.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kutaja mifano ya vyakula vya kiasili
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi
- ana changamoto katika kutumia angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo