Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutamka sauti nne za herufi moja ili kuimarisha mazungumzo,  
  2. kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika kujenga stadi ya kusikiliza,
  3. kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusikiliza,
  4. kusoma herufi za sauti moja katika kujenga stadi ya kusoma,
  5. kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma,
  6. kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma,
  7. kuandika herufi zinazowakilishwa na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kuandika,
  8. kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti zilizofunzwa katika mawasiliano ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi atamke sauti /g/, /d/, /j/, na /r/ katika maneno.
  • Mwanafunzi asikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha atamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili na kama darasa.
  • Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno.
  • Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kusikiliza matamshi ya sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atambue herufi zinazowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi.
  • Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno.
  • Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
  • Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kwa kuyagawa maneno marefu katika sehemu fupi fupi.
  • Mwanafunzi aandike herufi za  sauti alizosoma hewani na vitabuni.
  • Mwanafunzi aweza  kufinyanga maumbo ya herufi.
  • Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa wakiwa wawili wawili. 
  • Mwanafunzi aweza kutumia  vifaa vya kiteknolojia kama vile tarakilishi, projekta na kipasasauti kusikiliza na kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa.
  • Mwanafunzi aandike maumbo ya herufi na maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa.
  • Mwanafunzi asikilize imla inayojumuisha maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na kuyaandika.

MASWALI DADISI

  1. Je, ni sauti zipi unazojua kutamka?
  2. Unajua kusoma herufi  na maneno gani?
  3. Unajua kuandika herufi na maneno gani?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza kujiamini/kujithamini –  kuigiza na kusimulia.

Uhusiano na masuala mtambuko na maadili: 

uraia – utangamano wa kijamii  wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.   

Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages Activities  na Environmental activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na mashairi kuhusu shule.

 Uhusiano na Maadili:  

Uwajibikaji.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa shule.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuuliza maswali kuhusu shuleni  
  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia –ako na -enu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini  

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ukakamavu na ufasaha
  • anatumia msamiati wa shuleni katika sentensi ifaavyo na kwa ubunifu
  • anasoma kwa ufasaha
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini kwa ubunifu katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
  • anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anatumia msamiati wa shuleni ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini ifaavyo katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

 . 

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa shuleni katika sentensi
  • ana changamoto kiasi katika kusoma
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • ana changamoto katika kutumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa 
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa shuleni kwenye sentensi
  • ana changamoto nyingi katika kusoma
  • ana changamoto katika kutumia majina ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi 
  • ana changamoto katika kutumia ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • ana changamoto katika kuandika.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *