MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua maneno yatumiwayo katika maamkuzi ya nyakati za siku shuleni kwa mawasiliano mwafaka,
- kuamkua na kuitikia maamkuzi ya nyakati za siku shuleni katika kuimarisha mawasiliano,
- kusoma maneno yanayotumiwa katika maamkuzi shuleni katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kufafanua umuhimu wa salamu shuleni ili kuimarisha mawasiliano,
- kufurahia kuamkua wenzake, wafanyakazi na walimu shuleni katika kujenga mshikamano wa kijamii.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aigize maamkuzi mbalimbali ya nyakati za siku k.m habari ya asubuhi, jioni, mchana, umeamkaje na umeshindaje.
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa mchoro wa watu wawili wakisalimiana halafu aongozwe katika kujadili picha.
- Wanafunzi wasalimiane na kisha washirikishwe katika mjadala kuhusu maamkuzi.
- Wanafunzi waweza kuwekwa katika vikundi ili wajadili umuhimu wa maamkuzi.
- Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha watu wakitumia maamkuzi ya nyakati za siku.
- Mwanafunzi asome maamkuzi ya nyakati za siku katika kadi na chati.
MASWALI DADISI
- Tunaamkuana vipi wakati wa asubuhi, mchana na jioni?
- Kwa nini tunasalimiana shuleni?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza kujiamini/kujithamini – kuigiza na kusimulia.
Uhusiano na masuala mtambuko na maadili:
uraia – utangamano wa kijamii wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.
Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages Activities na Environmental activities.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- nyimbo na mashairi kuhusu shule.
Uhusiano na Maadili:
Uwajibikaji.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa shule.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuuliza maswali kuhusu shuleni
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia –ako na -enu katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ukakamavu na ufasaha
- anatumia msamiati wa shuleni katika sentensi ifaavyo na kwa ubunifu
- anasoma kwa ufasaha
- anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini kwa ubunifu katika sentensi
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
- anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anatumia msamiati wa shuleni ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini ifaavyo katika sentensi
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa shuleni katika sentensi
- ana changamoto kiasi katika kusoma
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa shuleni kwenye sentensi
- ana changamoto nyingi katika kusoma
- ana changamoto katika kutumia majina ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi
- ana changamoto katika kutumia ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kuandika.