Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua kwa kutaja msamiati wa shuleni katika kuimarisha umilisi wa lugha,
  2. kutumia msamiati wa shuleni katika mawasiliano ya kila siku, 
  • kusoma maneno na sentensi zinazojumuisha msamiati wa

shuleni katika kuimarisha stadi ya kusoma,

  • kuandika maneno na sentensi fupi kuhusu shule ili kuimarisha stadi ya kuandika,
  • kufurahia kutumia msamiati wa shule katika mawasiliano ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi aonyeshwe  vifaa halisi, picha au michoro ya vitu vinavyopatikana shuleni kama vile ofisi, maktaba, vyoo, darasa, bendera na gwaride.
  • Mwanafunzi achore maumbo ya vifaa vinavyopatikana shuleni.
  • Wanafunzi waambatanishe kadi za maneno na vifaa halisi  wakiwa katika vikundi.
  • Wanafunzi waweza kushiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu shule.
  • Mwanafunzi aandike majina ya vitu vinavyopatikana shuleni.
  • Mwanafunzi asome  msamiati wa shuleni katika kadi au chati.
  • Mwanafunzi atunge na kusoma  sentensi zinazojumuisha msamiati wa shuleni. 

MASWALI DADISI

  1. Je, unajua vifaa gani vinavyopatikana shuleni?
  2. Taja vifaa mbalimbali vinavyopatikana shuleni na umuhimu wake.

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza kujiamini/kujithamini –  kuigiza na kusimulia.

Uhusiano na masuala mtambuko na maadili: 

uraia – utangamano wa kijamii  wanafunzi watangamane na kufanya kazi pamoja.   

Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages Activities  na Environmental activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na mashairi kuhusu shule.

 Uhusiano na Maadili:  

Uwajibikaji.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa shule.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuuliza maswali kuhusu shuleni 
  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia –ako na -enu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini  

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ukakamavu na ufasaha
  • anatumia msamiati wa shuleni katika sentensi ifaavyo na kwa ubunifu
  • anasoma kwa ufasaha
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini kwa ubunifu katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo kila wakati
  • anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anatumia msamiati wa shuleni ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anatumia nambari kumi na moja hadi hamsini ifaavyo katika sentensi
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

 . 

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa shuleni katika sentensi
  • ana changamoto kiasi katika kusoma
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • ana changamoto katika kutumia -ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa 
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa shuleni kwenye sentensi
  • ana changamoto nyingi katika kusoma
  • ana changamoto katika kutumia majina ya nambari kutoka kumi na moja hadi hamsini kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi 
  • ana changamoto katika kutumia ako na -enu kutunga sentensi ifaavyo
  • ana changamoto katika kuandika.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *