Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua matumizi ya –angu na –etu katika mawasiliano,
 2. kutumia –angu na – etu katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano,
 3. kufurahia kutumia  –angu na – etu katika mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi atunge sentensi zenye matumizi ya angu na –etu.
 • Mwanafunzi aandike sentensi zenye kuhusisha –angu na –etu.
 • Mwanafunzi asome sentensi zenye kutumia maneno angu na –etu.
 • Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia angu na –etu.
 • Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la kujaza mapengo kwa tarakilishi (mchezo wa kuvuta na kutia kapuni).

MASWALI DADISI

 1. Je, ni maneno gani tunayotumia
 2. kuonyesha kuwa kitu ni chako au ni chenu?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:

 • mawasiliano na ushirikiano –  kujadili katika makundi au wawili wawili
 • hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kujua vyakula zaidi
 • ujuzi wa kidijitali –matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya afya: magonjwa yanayohusiana na vyakula  – kuthamini vyakula vya kiasili.

Uhusiano na Masomo mengine:  

Health and Nutrition Activities na Environmental Activities

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

 • kazi ya vikundi 
 • michezo

nyimbo na Mashairi kuhusu vyakula vya kiasili

 Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuuliza maswali kuhusu vyakula vya kiasili 
 • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa 
 • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
 • kuchunguza jinsi anavyotumia –angu na -etu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
 • anaelezea mifano ya vyakula vya

kiasili

 • anatumia msamiati wa  vyakula vya kiasili kwa ubunifu katika sentensi
 • anasoma kwa ufasaha
 • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
 • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • anaandika kwa hati nadhifu.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa vyema
 • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili 

 • anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili ifaavyo katika sentensi
 • anasoma ifaavyo
 • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
 • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • anaandika kwa hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
 • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili

 • ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa  vyakula vya kiasili katika sentensi
 • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
 • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
 • ana changamoto katika kutumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • ana changamoto katika kusoma. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
 • ana changamoto katika kutaja mifano ya vyakula vya kiasili 
 • ana changamoto katika kutumia msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
 • ana changamoto katika kusoma
 • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi
 • ana changamoto katika kutumia angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *