Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi aliyosoma au kusomewa ili kuimarisha mawasiliano,
 2. kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu vyakula

vya kiasili ili kuimarisha stadi ya kusoma,

 • kusoma hadithi kuhusu vyakula vya kiasili katika kuimarisha stadi ya kusoma,
 • kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa kuhusu vyakula vya

kiasili ili kupata ujumbe unaolengwa,

e) kufurahia vyakula vya kiasili maishani.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
 • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
 • Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
 • Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu kisha asome peke yake, wawili wawili au katika vikundi.
 • Mwanafunzi asikilize hadithi ya mwalimu au hadithi iliyorekodiwa kuhusu vyakula vya kiasili.
 • Mwanafunzi aweza  kusoma na kusomewa hadithi kupitia vifaa vya kiteknolojia kama vile  tarakilishi, projekta n.k.
 • Mwanafunzi aweza  kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa. 
 • Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa hadithi.
 • Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi.
 • Wanafunzi aulize na kujibu maswali kutokana na hadithi.

MASWALI DADISI

 1. Je, unaona nini  katika picha?
 2. Unadhani ni nini kitakachotokea katika hadithi?
 • Unakumbuka hadithi gani uliyoisoma?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:

 • mawasiliano na ushirikiano –  kujadili katika makundi au wawili wawili
 • hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atajenga msingi wa kujua vyakula zaidi
 • ujuzi wa kidijitali –matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya afya: magonjwa yanayohusiana na vyakula  – kuthamini vyakula vya kiasili.

Uhusiano na Masomo mengine:  

Health and Nutrition Activities na Environmental Activities

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

 • kazi ya vikundi 
 • michezo

nyimbo na Mashairi kuhusu vyakula vya kiasili

Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuuliza maswali kuhusu vyakula vya kiasili 
 • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa 
 • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
 • kuchunguza jinsi anavyotumia –angu na -etu katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
 • anaelezea mifano ya vyakula vya

kiasili

 • anatumia msamiati wa  vyakula vya kiasili kwa ubunifu katika sentensi
 • anasoma kwa ufasaha
 • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
 • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • anaandika kwa hati nadhifu.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti lengwa vyema
 • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili 

 • anatumia msamiati wa vyakula vya kiasili ifaavyo katika sentensi
 • anasoma ifaavyo
 • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
 • anatumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • anaandika kwa hati bora.

 .  Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
 • anataja mifano ya vyakula vya

kiasili

 • ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa  vyakula vya kiasili katika sentensi
 • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
 • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
 • ana changamoto katika kutumia -angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo
 • ana changamoto katika kusoma. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa vyema
 • ana changamoto katika kutaja mifano ya vyakula vya kiasili 
 • ana changamoto katika kutumia msamiati wa vyakula vya kiasili katika sentensi
 • ana changamoto katika kusoma
 • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi
 • ana changamoto katika kutumia angu na -etu kutunga sentensi ifaavyo

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *