MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati wa dukani ili kuutumia katika mawasiliano,
- kusoma maneno yanayohusiana na shughuli za dukani ili kujenga usomaji bora,
- kueleza maana ya msamiati wa dukani ili kuimarisha stadi ya
kuzungumza,
- kutumia msamiati wa dukani katika sentensi sahihi ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
- kuandika maneno yanayohusiana na uuzaji na ununuzi ili kuimarisha stadi ya kusoma,
- kuthamini shughuli za biashara.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na shughuli za dukani kwa kutumia kadi za maneno kama vile nunua, uza, bei, kilo, mnunuzi, mwuzaji, hasara, faida, pesa, baki, sarafu na noti.
- Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu maana ya maneno yanayohusiana na shughuli za dukani kwa kutumia picha au michoro.
- Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa dukani.
- Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu uuzaji na ununuzi.
- Wanafunzi washiriki katika majadiliano kuhusu umuhimu wa kufanya biashara wakiwa kwenye vikundi.
MASWALI DADISI
- Mtu anayenunua kitu dukani huitwaje?
- Mtu anayeuza dukani huitwaje?
Pesa unazorudishiwa unaponunua kitu dukani huitwaje?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya maswala ya kifedha katika ujuzi wa kutumia pesa vizuri.
stadi za maisha – Kuwa na ujasiri wa kwenda na kufanya maamuzi mwafaka ya ununuzi.
Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities na English Activitites.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani shuleni kushiriki katika majadiliano kuhusu bidhaa zinazopatikana dukani.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji – Kuweza kuwa mwadilifu katika matumizi ya pesa dukani.
ushirikiano – Kufanya kazi katika vikundi.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuweza kutumwa dukani na wazazi na kutumia pesa inavyofaa.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa dukani katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia alama ya kuuliza katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa
- kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
• kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia msamiati wa dukani ipasavyo
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ubunifu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika maandishi kila inapohitajika
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua msamiati wa dukani
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
- anafahamu anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika maandishi
- anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua baadhi ya msamiati wa dukani.
- anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
- anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani
- anafahamu baadhi ya mambo anayosoma au kusomewa
- anatumia alama ya kuuliza katika baadhi ya sentensi
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutambua baadhi ya msamiati wa dukani
- ana changamoto katika kusimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
- ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto katika kuakifisha sentensi kwa kutumia alama ya kuuliza
- ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyofunzwa.