CBC Grade 1 Kiswahili Sub strand 2.1
MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua wenzake darasani kwa majina, jinsia, miaka na gredi ili kuweza kuwaelezea,
- kujieleza kwa kurejelea jina, jinsia, miaka na gredi kwa ufasaha katika mawasiliano ya kila siku,
- kutoa muhtasari wa maelezo aliyoyasikiliza katika mazingira yake,
- kudhihirisha umakinifu wa kusikiliza katika mazingira yake,
- kuchangamkia maelezo yake na ya wenzake katika kuimarisha mawasiliano,
- kujivunia nafsi yake na wenzake katika miktadha mbalimbali.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi asikilize maelezo ya wengine.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza maelezo ya wenzake yaliyorekodiwa kwenye simu, kinasa sauti, kipatakalishi n.k.
- Wanafunzi watoleane maelezo kuwahusu katika vikundi.
- Wanafunzi wakiwa wawili wawili waulizane maswali na kujibizana k.m. Unaitwaje?
- Mwanafunzi atoe maelezo yake akizingatia jina, jinsia, umri na gredi mbele ya darasa.
- Mwanafunzi aeleze maana ya msamiati unaotumiwa kujieleza k.v. umri, miaka,msichana, mvulana, gredi na rafiki.
- Mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia maneno yanayotumiwa kujieleza na kueleza wenzake.
- Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu maana na matumizi ya msamiati unaotumiwa k.m. umri, miaka, msichana, mvulana, gredi na rafiki katika vikundi.
MASWALI DADISI
- Wewe ni nani?
- Unajua mambo yapi kuhusu mwenzako?
- Unapenda kufanya nini?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
Mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu katika kujieleza darasani. Vilevile wanashiriki katika kazi ya vikundi Ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza
Uhusiano na masuala mtambuko: Stadi za maisha: kujitambua na kujithamini kijamii wanapojieleza
Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni.
Uhusiano na Maadili: Heshima kwa wengine
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kujizatiti kuwajua wenzake shuleni na vijijini kuwafunza wenzake umuhimu wa kuwajua watu katika mazingira yao kwa majina kwa usalama wao.
Mapendekezo ya Tathmini:
kuchunguza ukakamavu wa mwanafunzi anapojieleza kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- ufasaha
- anaelezea wenzake kwa anajieleza kwa ukakamavu na
- ukakamavu na ufasaha
- anasimulia kisa kwa lugha ifaayo na yenye ubunifu
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa kwa ubunifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anajieleza kwa ufasaha
- anaelezea wenzake kwa ufasaha
- anasimulia kisa kwa lugha ifaayo
- anajibu maswali ya ufahamu kwa usahihi
- anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anajieleza ifaavyo
- anaelezea wenzake ifaavyo
- anasimulia baadhi ya visa
- ana changamoto katika kujibu baadhi maswali kutokana na hadithi
- ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kujieleza ifaavyo
- ana changamoto katika kuelezea wenzake ifaavyo
- ana changamoto katika kusimulia
kisa
- ana changamoto katika kujibu maswali mengi kutokana na hadithi
- ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.