Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kusimulia hadithi aliyosikiliza darasani ili kujenga stadi ya kusikiliza, 
  2. kufahamu hadithi aliyosimuliwa ili kupata ujumbe,
  3. kuonyesha umakinifu wa kusikiliza katika miktadha mbalimbali, 
  4. kuchangamkia hadithi simulizi maishani.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi aweze kuwa makini anaposimuliwa masimulizi kwa kumtazama msemaji na kutofanya lolote anaposikiliza miongni mwa mengine.
  • Mwanafunzi asikilize masimulizi kupitia vifaa vya teknolojia k.m. simu, kinasa sauti, kipatakalishi n.k.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa akisimulia masimulizi.
  • Wanafunzi waweza kuwekwa katika vikundi na kutoleana muhtasari wa masimulizi yaliyosimuliwa.
  • Mwanafunzi aulize na kujibu maswali kutokana na masimulizi.

MASWALI  DADISI

  1. Umewahi kusimuliwa kisa kipi?
  2. Unatarajiwa kufanya nini unaposimuliwa kisa?
  3. Unakumbuka nini katika masimulizi uliyosimuliwa?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

Mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu katika kujieleza darasani. Vilevile wanashiriki katika kazi ya vikundi Ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza

Uhusiano na masuala mtambuko: Stadi za maisha:  kujitambua na kujithamini kijamii wanapojieleza 

Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages na Religious Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kazi ya vikundi  shughuli za vikundi vya ushirika shuleni.

 Uhusiano na Maadili: Heshima kwa wengine 

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kujizatiti kuwajua wenzake shuleni na vijijini kuwafunza wenzake umuhimu wa kuwajua watu katika mazingira yao kwa majina kwa usalama wao.

Mapendekezo ya Tathmini:

kuchunguza  ukakamavu wa mwanafunzi anapojieleza  kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi.

 

 

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • ufasaha
  • anaelezea wenzake kwa anajieleza kwa ukakamavu na
  • ukakamavu na ufasaha
  • anasimulia kisa kwa lugha ifaayo na yenye ubunifu
  • anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa kwa ubunifu.

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anajieleza kwa ufasaha 
  • anaelezea wenzake kwa ufasaha
  • anasimulia kisa kwa lugha ifaayo
  • anajibu maswali ya ufahamu kwa usahihi
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anajieleza ifaavyo
  • anaelezea wenzake ifaavyo
  • anasimulia baadhi ya visa 
  • ana changamoto katika  kujibu baadhi maswali kutokana na hadithi
  • ana changamoto katika  kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika  kujieleza ifaavyo
  • ana changamoto katika  kuelezea wenzake ifaavyo
  • ana changamoto katika kusimulia

kisa

  • ana changamoto katika kujibu maswali mengi kutokana na hadithi
  • ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.

Grade one Kiswahili Curriculum Designs: Sub strand 2.2-kusikiliza na kuzungumza :Masimulizi

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *