MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati uliyotumika katika hadithi ili kuweza kuutumia katika mawasiliano,
- kusikiliza hadithi zikisomwa ili kujenga usikivu,
- kufahamu hadithi aliyosomewa darasani ili kupata ujumbe,
- kuchangamkia kusikiliza hadithi kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusomewa hadithi.
- Mwanafunzi aeleze matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Wanafunzi wajadiliane kuhusu hadithi waliosomewa katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi zikisomwa kupitia vifaa vya teknolojia k.v. tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa picha na kadi za msamiati uliotumiwa katika hadithi.
• Mwanafunzi aulize na kujibu maswali kutokana na hadithi.
MASWALI DADISI
- Je, ni hadithi gani ambayo umewahi kusomewa?
- Unatarajiwa kufanya nini unaposomewa hadithi?
- Unakumbuka nini katika hadithi uliyosomewa?
- Unafikiria ni nini kitakachotokea katika hadithi hii?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
Mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu katika kujieleza darasani. Vilevile wanashiriki katika kazi ya vikundi Ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza
Uhusiano na masuala mtambuko: Stadi za maisha: kujitambua na kujithamini kijamii wanapojieleza
Uhusiano na masomo mengine: English Activities, Literacy and Indigenous Languages na Religious Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni.
Uhusiano na Maadili: Heshima kwa wengine
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kujizatiti kuwajua wenzake shuleni na vijijini kuwafunza wenzake umuhimu wa kuwajua watu katika mazingira yao kwa majina kwa usalama wao.
Mapendekezo ya Tathmini:
kuchunguza ukakamavu wa mwanafunzi anapojieleza kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- ufasaha
- anaelezea wenzake kwa anajieleza kwa ukakamavu na
- ukakamavu na ufasaha
- anasimulia kisa kwa lugha ifaayo na yenye ubunifu
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa kwa ubunifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anajieleza kwa ufasaha
- anaelezea wenzake kwa ufasaha
- anasimulia kisa kwa lugha ifaayo
- anajibu maswali ya ufahamu kwa usahihi
- anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anajieleza ifaavyo
- anaelezea wenzake ifaavyo
- anasimulia baadhi ya visa
- ana changamoto katika kujibu baadhi maswali kutokana na hadithi
- ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kujieleza ifaavyo
- ana changamoto katika kuelezea wenzake ifaavyo
- ana changamoto katika kusimulia
kisa
- ana changamoto katika kujibu maswali mengi kutokana na hadithi
- ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa.