Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua nambari moja hadi kumi

(1-10) katika mazingira yake, 

  • kuhesabu nambari 1-10 kwa mfuatano ili kujenga stadi ya kuzungumza,
  • kutaja majina ya nambari moja hadi kumi kwa mfululizo ili kujenga stadi ya kuzungumza,
  • kutumia majina ya nambari moja hadi kumi kutunga sentensi ili kujenga stadi ya kuzungumza,
  • kuthamini matumizi ya nambari katika maisha ya kila siku. 

 MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi anaweza kupewa kadi za nambari azitaje kwa maneno.
  • Mwanafunzi aweza  kukariri mashairi kuhusu nambari moja hadi kumi.
  • Mwanafunzi aweza kushirikishwa kuimba nyimbo za tarakimu.
  • Wanafunzi waambatanishe nambari na maneno kwa kuonyeshwa nambari na kutaja jina la nambari husika.
  • Wanafunzi wahesabu vidole kwa Kiswahili wakiwa wawili wawili k.m. mmoja anachukua kidole kimoja na mwingine anataja jina la nambari, kwa mfano, kidole kimoja kiambatane na neno ‘moja’ n.k.
  • Wanafunzi wanaweza kupanga kadi za majina ya nambari moja hadi kumi kwa utaratibu.
  • Mwanafunzi aweza kuonyeshwa nambari na jina kwa kutumia tarakilishi na projekta.
  • Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video ya wanafunzi wakisoma nambari moja hadi kumi kwa tarakilishi. 

MASWALI  DADISI

  1. Unajua kuhesabu nambari ngapi? 
  2. Hesabu moja hadi kumi.
  3. Unaweza kutumia majina yapi ya nambari moja hadi kumi katika sentensi?
  4. Ni nini umuhimu wa nambari maishani?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashiriki katika kazi ya vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza

hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atapata hamu ya kuendelea kuhesabu kwa kutumia Kiswahili

Uhusiano na masuala mtambuko: Stadi za maisha:  kujitambua wanapohesabu viungo vya mwili.

Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kazi ya vikundi  shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi

 Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji wa kutunza alicho nacho na cha wenzake. 

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kutumia ujuzi wa kuhesabu katika biashara hasa anapotumwa dukani au sokoni.

 Mapendekezo ya Tathmini:

kuchunguza  uwezo wa kuhesabu kwa Kiswahili  kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana hesabu moja hadi kumi kwa haraka
  • anatumia msamiati wa nambari kwa ubunifu katika sentensi
  • anasimulia kisa kwa ufasaha na ubunifu
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa kwa ubunifu.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi ,

  • anahesabu moja hadi kumi
  • anatumia msamiati wa nambari katika sentensi ifaavyo
  • Anasimulia kisa kwa ufasaha. 
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana changamoto chache katika kuhesabu moja hadi kumi
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa nambari katika sentensi
  • anasimulia baadhi ya visa
  • ana changamoto katika  kujibu baadhi ya maswali ya ufahamu kwenyehadithi na masimulizi
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana changamoto nyingi katika kuhesabu moja hadi kumi
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa nambari katika sentensi
  • ana changamoto katika kusimulia

kisa 

  • ana changamoto katika  kujibu maswali mengi kutokana na hadithi na masimulizi
  • ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

Kiswahili Grade 1 Curriculum Design Sub strand 3.1-kusikiliza na kuzungumza: Msamiati

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *