Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kusikiliza visa vinavyohusiana na nambari ili kujenga umakinifu, 
  2. kufahamu masimulizi ya visa vinavyohusiana na nambari ili kupata ujumbe,
  3. kuonyesha umakinifu wa kusikiliza katika mawasiliano, 
  4. kuchangamkia masimulizi katika maisha ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi asikilize kisa kikisimuliwa.
  • Mwanafunzi ashiriki katika kusimulia kisa kinachohusisha nambari.
  • Mwanafunzi atoe muhtasari wa matukio yaliyosimuliwa. 
  • Wanafunzi waweza kusimuliana visa vinavyojumuisha nambari wakiwa wawili wawili au katika vikundi.

Mwanafunzi aweza kusikiliza masimulizi kupitia kwa vyombo vya kiteknolojia kama vile simu, kinasasauti na kipatakalishi vyaweza kutumiwa katika kusimulia visa mbalimbali. 

MASWALI  DADISI

  1. Nambari hutumiwaje?
  2. Unatarajiwa kufanya nini unaposimuliwa kisa?
  3. Unakumbuka nini katika kisa ulichosimuliwa?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – Wanatumia lugha faafu darasani. Vilevile wanashiriki katika kazi ya vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza

hamu ya ujifunzaji: mwanafunzi atapata hamu ya kuendelea kuhesabu kwa kutumia Kiswahili

Uhusiano na masuala mtambuko: Stadi za maisha:  kujitambua wanapohesabu viungo vya mwili.

Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kazi ya vikundi  shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi

 Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji wa kutunza alicho nacho na cha wenzake. 

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: 

kutumia ujuzi wa kuhesabu katika biashara hasa anapotumwa dukani au sokoni.

 Mapendekezo ya Tathmini:

kuchunguza  uwezo wa kuhesabu kwa Kiswahili  kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana hesabu moja hadi kumi kwa haraka
  • anatumia msamiati wa nambari kwa ubunifu katika sentensi
  • anasimulia kisa kwa ufasaha na ubunifu
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa kwa ubunifu.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi ,

  • anahesabu moja hadi kumi
  • anatumia msamiati wa nambari katika sentensi ifaavyo
  • Anasimulia kisa kwa ufasaha. 
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi 
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana changamoto chache katika kuhesabu moja hadi kumi
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa nambari katika sentensi
  • anasimulia baadhi ya visa
  • ana changamoto katika  kujibu baadhi ya maswali ya ufahamu kwenyehadithi na masimulizi
  • anatoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi ,

  • ana changamoto nyingi katika kuhesabu moja hadi kumi
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa nambari katika sentensi
  • ana changamoto katika kusimulia

kisa 

  • ana changamoto katika  kujibu maswali mengi kutokana na hadithi na masimulizi
  • ana changamoto katika kutoa muhtasari wa hadithi aliyosimuliwa au kusomewa.

CBC Grade 1 Kiswahili Curriculum Designs-3.0-Sub Strand-3.2-kusikiliza na kuzungumza: Masimulizi

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *