MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati uliotumika katika hadithi ili kuimarisha ufahamu,
kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu zinazojumuisha matukio ya siku za wiki ili kujenga umakinifu,
- kufahamu hadithi aliyosomewa katika mada ili kupata ujumbe,
- kuchangamkia kusikiliza hadithi kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusomewa hadithi.
- Mwanafunzi asikilize hadithi ikisomwa na mwalimu.
- Mwanafunzi aeleze matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu hadithi waliyosomewa katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kushirikishwa kusikiliza hadithi kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia k.v. tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa picha na kadi za maneno yaliyotumiwa katika hadithi.
- Mwanafunzi ajibu na aulize maswali kutokana na hadithi.
MASWALI DADISI
- Umewahi
kusikiliza hadithi ipi?
- Unatarajiwa kufanya nini unaposomewa hadithi?
- Unafikiri ni nini kitakachotokea katika hadithi?
- Unakumbuka hadithi ipi uliyosomewa?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kazi za vikundi ujuzi wa kidijitali : kuandika kwa vipakatalishi na kusikiliza visa ubunifu: kueleza namna ya kutumia kila siku aliyo nayo.
Uhusiano na masuala mtambuko: stadi za Maisha (uwajibikaji) -kufanya uamuzi wa jinsi ya kutumia siku za wiki uzalendo: kushirikiana katika vikundi.
Uhusiano na Masomo mengine: Literacy activities, Religious Activities na
Mathematics Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo nyimbo na mashairi kuhusu siku za wiki.
Uhusiano na Maadili:
heshima kwa siku zilizotengewa shughuli za kidini.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kusisitiza umuhimu wa shughuli tofauti kwa mfano siku za kwenda shule, siku ya kupumzika na siku ya kwenda maabadini kwa wenzake na miongoni mwa wanajamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyoorodhesha siku za wiki na kuzitungia sentensi
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anaorodhesha siku za wiki kwa haraka na ifaavyo
- anatumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano kwa ubunifu
- anasimulia kisa kwa ufasaha na ubunifu
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anaorodhesha siku za wiki ifaavyo
- anatumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- anasimulia kisa kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi kwa usahihi.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika orodhesha siku za wiki ifaavyo
- ana changamoto katika kutumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- anasimulia baadhi ya visa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto nyingi katika kuorodhesha siku za wiki
- ana changamoto nyingi katika kutumia majina ya siku za wiki katika mawasiliano
- Ana changamoto katika kusimulia
visa
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu wa hadithi na masimulizi.