MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutamka sauti nne za herufi moja ili kuimarisha mazungumzo,
- kutambua sauti za herufi moja zilizofunzwa katika maneno ili kuimarisha mazungumzo,
- kutambua majina ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kusoma,
- kusoma herufi za sauti moja katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma maneno kwa kutumia
silabi zinazotokana na sauti lengwa katika kujenga stadi ya kusoma,
- kusoma vifungu vilivyo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kujenga stadi ya
kusoma,
- kuandika maumbo ya herufi zinazowakilisha sauti lengwa katika kuimarisha stadi ya kuandika,
- kuchangamkia kutumia maneno yanayojumuisha sauti
zilizofunzwa katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ashirikishwe kutambua sauti /m/, /a/, /u/ na /k/ katika maneno.
- Mwanafunzi asikilize mwalimu akitamka sauti lengwa, kisha watamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili wawili na katika darasa.
- Mwanafunzi atumie teknolojia (papaya) kutamkia sauti.
- Mwanafunzi atambue herufi inayowakilisha sauti lengwa kwa kutumia kadi za herufi.
- Mwanafunzi aambatanishe silabi kusoma maneno yanayotokana na sauti lengwa.
- Mwanafunzi atenganishe silabi katika kutambua sehemu mbalimbali za maneno.
- Wanafunzi waweza kushirikishwa kusikiliza mgeni mwalikwa mwenye umahiri wa kutamka sauti lengwa.
- Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi au kugawa maneno marefu zaidi vipande vipande.
- Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa kama darasa au wawili wawili.
- Mwanafunzi asikilize na kusoma hadithi kupitia vifaa vya teknolojia kama vile tarakilishi, projekta n.k.
- Mwanafunzi afinyange na aandike maumbo ya herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni.
- Mwanafunzi aandike maneno yaliyo na herufi za sauti alizofunzwa kwa kunakili aliyoandika mwalimu.
MASWALI DADISI
- Ni sauti zipi unazojua kutamka?
- Unajua kusoma herufi na maneno yapi?
- Unajua kuandika herufi na maneno yapi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
- mawasiliano na ushirikiano – Kujadiliana kuhusu majukumu ya watu wa familia; Kufanya kazi kwa vikundi
- hamu ya ujifunzaji: Matumizi ya nafsi ya kwanza wakati uliopo
- ujuzi wa kidijitali :Kuna mapendekezo ya kutumia vifaa vya kiteknolojia kufunzia
- ubunifu: Utunzi wa sentensi kwa kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo.
Uhusiano na masuala mtambuko:
- uraia: uzalendo: kushirikiana katika vikundi
- utangamano wa kijamii – mahusiano katika familia.
Uhusiano na masomo mengine: Religious Studies, English Activities na Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo.
Mahusiano na Maadili:
mapenzi na heshima katika familia.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kutembelea nyumba ya mayatima na kucheza nao kuwaelimisha wengine umuhimu wa familia katika ujenzi wa jamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyowatambua watu katika familia yake
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia nafsi ya kwanza wakati uliopo katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia zaidi ya aliyofunzwa
- anatumia majina ya watu wa familia kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi zenye ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa familia katika sentensi ifaavyo
- anasoma hadithi
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati inayosomeka.
. Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa
familia katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- anaandika kwa hati inayosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- ana changamoto katika kutumia majina ya watu wa familia katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.