MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua maneno ya heshima katika mawasiliano,
- kutumia maneno ya heshima katika mawasiliano,
- kuambatanisha maneno ya heshima na hisia zifaazo katika mawasiliano,
- kuthamini matumizi ya maneno ya heshima katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Wanafunzi waweza kuonyeshwa mchoro wa mtoto akipokea zawadi halafu wajadili neno linalofaa kutumiwa na anayepokea zawadi.
- Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video inayoashiria matumizi ya maneno ya heshima k.m. Mtu akipokea zawadi au wageni wakimtembelea mgonjwa hospitalini.
- Mwanafunzi aweza kupewa ufafanuzi kuhusu maneno ya heshima kama vile “asante, pole na tafadhali.”
- Wanafunzi waweza kushirikishwa katika kuigiza vitendo vya heshima.
- Mwanafunzi ahusishwe katika mjadala kuhusu umuhimu wa kutumia maneno ya heshima.
MASWALI DADISI
- Unapopewa zawadi unatakiwa kusema nini?
- Mwenzako anapojikwaa utamwambiaje?
- Unapoomba ruhusu kutoka kwa mwalimu unatumia neno gani?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
- mawasiliano na ushirikiano – Kujadiliana kuhusu majukumu ya watu wa familia; Kufanya kazi kwa vikundi
- hamu ya ujifunzaji: Matumizi ya nafsi ya kwanza wakati uliopo
- ujuzi wa kidijitali :Kuna mapendekezo ya kutumia vifaa vya kiteknolojia kufunzia
- ubunifu: Utunzi wa sentensi kwa kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo.
Uhusiano na masuala mtambuko:
- uraia: uzalendo: kushirikiana katika vikundi
- utangamano wa kijamii – mahusiano katika familia.
Uhusiano na masomo mengine: Religious Studies, English Activities na Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo.
Mahusiano na Maadili:
mapenzi na heshima katika familia.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kutembelea nyumba ya mayatima na kucheza nao kuwaelimisha wengine umuhimu wa familia katika ujenzi wa jamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyowatambua watu katika familia yake
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia nafsi ya kwanza wakati uliopo katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia zaidi ya aliyofunzwa
- anatumia majina ya watu wa familia kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi zenye ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa familia katika sentensi ifaavyo
- anasoma hadithi
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati inayosomeka.
. Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa
familia katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- anaandika kwa hati inayosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- ana changamoto katika kutumia majina ya watu wa familia katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.