MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati uliotumika katika hadithi,
- kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu zinazohusu familia darasani,
- kusoma hadithi kuhusu familia darasani,
- kufahamu hadithi aliyosomewa kuhusu familia darasani,
- kuchangamkia kusikiliza hadithi kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
• Mwanafunzi aweza kujadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi aweza kutabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi aweza kufuatilia hadithi ikisomwa na mwalimu, kisha asome pamoja na mwalimu na baadaye asome akiwa peke yake au wawili wawili.
- Mwanafunzi aweza kueleza maana na matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi ukiwemo msamiati wa familia kama vile baba, mama, kaka na dada.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu na kisha asome peke yake, wawili wawili au katika vikundi.
- Mwanafunzi asikilize hadithi ya mwalimu au iliyorekodiwa inayojumuisha matumizi ya maneno ya heshima.
- Mwanafunzi aweza kutoa muhtasari wa hadithi aliyosoma au aliyosomewa.
- Wanafunzi waweza kutunga sentensi wakitumia majina ya watu wa familia katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa.
- Mwanafunzi aweza kuthibitisha utabiri wake baada ya kusomewa hadithi.
- Wanafunzi waweza kushirikishwa katika kuuliza na kujibu maswali kutokana na hadithi darasani na vilevile kuyaandika kwenye madaftari yao.
MASWALI DADISI
- Unakumbuka nini katika hadithi uliyosomewa?
- Unaweza kutabiri kitakachotokea katika hadithi?
- Unaweza kusoma hadithi?
- Kwa nini unapenda hadithi?
- Unakumbuka hadithi gani uliyosoma?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
- mawasiliano na ushirikiano – Kujadiliana kuhusu majukumu ya watu wa familia; Kufanya kazi kwa vikundi
- hamu ya ujifunzaji: Matumizi ya nafsi ya kwanza wakati uliopo
- ujuzi wa kidijitali :Kuna mapendekezo ya kutumia vifaa vya kiteknolojia kufunzia
- ubunifu: Utunzi wa sentensi kwa kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo.
Uhusiano na masuala mtambuko:
- uraia: uzalendo: kushirikiana katika vikundi
- utangamano wa kijamii – mahusiano katika familia.
Uhusiano na masomo mengine: Religious Studies, English Activities na Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kazi ya vikundi shughuli za vikundi vya ushirika shuleni michezo.
Mahusiano na Maadili:
mapenzi na heshima katika familia.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:
kutembelea nyumba ya mayatima na kucheza nao kuwaelimisha wengine umuhimu wa familia katika ujenzi wa jamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza jinsi anavyowatambua watu katika familia yake
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia nafsi ya kwanza wakati uliopo katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia zaidi ya aliyofunzwa
- anatumia majina ya watu wa familia kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi zenye ubunifu
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa familia katika sentensi ifaavyo
- anasoma hadithi
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati inayosomeka.
. Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- anatumia majina ya watu wa
familia katika sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- anaandika kwa hati inayosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- anawataja watu wa familia
- ana changamoto katika kutumia majina ya watu wa familia katika sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- Ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia nafsi ya kwanza wakati uliopo kutunga sentensi
- ana changamoto katika kuandika.