MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutaja haki zake ili kuimarisha ufahamu wa masuala yanayomwathiri,
- kueleza umuhimu wa haki za watoto ili kutetea haki zake zinapokiukwa,
- kusimulia kuhusu haki zake ili kujenga stadi ya kuzungumza,
- kusikiliza masimulizi kuhusu haki za watoto ili kuimarisha umakinifu,
- kuthamini haki za watoto ili kuzitetea maishani.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ataje haki zake k.v. kuishi, elimu, kupewa malezi bora, matibabu, kutoteswa, kupewa jina, chakula na mavazi.
- Wanafunzi wajadili michoro, chati au picha zinazozingatia haki za watoto.
- Mwanafunzi aweza kusimulia kisa kuhusu haki za watoto.
- Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu haki za watoto.
- Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu haki za watoto.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa akizungumza kuhusu haki za watoto.
- Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu haki za watoto.
MASWALI DADISI
- Je, unajua haki zipi zinazokuhusu?
- Haki za watoto zinakusaidiaje?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika shughuli za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Uhusiano na masuala mtambuko: uraia – haki za watoto -wanafunzi wanahamasishwa kuhusu haki zake.
Uhusiano na Masomo mengine: Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- nyimbo na mashairi kuhusu haki za watoto.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji haki za kijamii heshima.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu haki za watoto.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuuliza maswali kuhusu haki za watoto
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia vizuri na vibaya katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema na kwa ukakamavu
- anatambua haki za watoto na kuzitilia maanani katika mawasiliano
- anatumia msamiati wa haki za watoto kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anatetea haki za watoto kwa ukakamavu
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo na kwa ubunifu wa hali ya juu.
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
- Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anatambua haki za watoto
- anatumia msamiati wa haki za watoto ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anatetea haki za watoto
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anatambua haki za watoto
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto kiasi katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
- Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutambua haki za watoto
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
- ana changamoto katika kusoma kazi anazopewa
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu kwenye hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kusoma.