Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua picha kuhusu haki za watoto ili kuifahamu hadithi vizuri,
  • kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu haki za watoto katika

kuimarisha stadi za  kusikiliza na kusoma,

  • kusoma hadithi kuhusu haki za watoto katika kuimarisha stadi ya kusoma,
  • kufahamu hadithi  aliyoisoma au aliyosomewa ili kupata mafunzo yanayolengwa,
  • kuchangamkia kusoma hadithi kuhusu haki za watoto ili kuendeleza stadi ya kusoma.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

  • Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi adhihirishe ufahamu wa matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na mwalimu na baadaye asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia k.m.  tarakilishi na projekta.
  • Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa jitabu mbele ya darasa. 
  • Mwanafunzi ajibu na  kuuliza maswali yanayotokana na hadithi aliyosoma au kusomewa.
  • Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.

MASWALI DADISI

  1. Ni masuala yapi uliyojifunza katika hadithi uliyosoma? 
  2. Ni haki zipi za watoto zimezingatiwa katika hadithi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika shughuli za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko:  uraia – haki za watoto -wanafunzi wanahamasishwa kuhusu haki zake.                   

Uhusiano na Masomo mengine: Environmental Activities

 Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • nyimbo na mashairi kuhusu haki za watoto.

 Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji haki za kijamii heshima.

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu haki za watoto.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuuliza maswali kuhusu haki za watoto 
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
  • kuchunguza jinsi anavyotumia vizuri na vibaya katika sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema na kwa ukakamavu
  • anatambua haki za watoto na kuzitilia maanani katika mawasiliano 
  • anatumia msamiati wa haki za watoto kwa ubunifu katika sentensi
  • anasoma kwa ufasaha
  • anatetea haki za watoto kwa ukakamavu
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi 
  • anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo na kwa ubunifu wa hali ya juu.
  • anaandika kwa hati nadhifu.

 Kufikia Matarajio

  • Mwanafunzi,
  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anatambua haki za watoto 
  • anatumia msamiati wa haki za watoto ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anatetea haki za watoto
  • anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo anaandika kwa hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • anatambua haki za watoto 
  • ana changamoto katika  kutumia baadhi ya msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
  • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
  • anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • ana changamoto  kiasi katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

  • Mwanafunzi,
  • ana changamoto katika  kutamka sauti lengwa
  • ana changamoto katika kutambua haki za watoto 
  • ana changamoto katika  kutumia msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kusoma kazi anazopewa
  • ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu kwenye  hadithi na masimulizi kwa usahihi
  • ana changamoto katika kutumia  vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
  • ana changamoto katika kusoma.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *