MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua matumizi yafaayo ya vizuri na vibaya katika mawasiliano
- kutumia vizuri na vibaya katika sentensi sahihi ili kuimarisha mawasiliano
- kusoma sentensi zinazojumuisha vizuri na vibaya ili kuimarisha usomaji bora
- kuandika sentensi kwa kujumuisha vizuri na vibaya ili kuimarisha uandishi mwafaka
e) kuchangamkia matumizi ya vizuri na vibaya katika kuimarisha mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia vizuri na vibaya.
- Mwanafunzi aweza kubainisha matumizi ya vielezi lengwa kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia.
- Mwanafunzi arejelee vitendo mbalimbali kwa kutumia vizuri na vibaya k.m Mtoto amesoma vizuri.
- Mwanafunzi aandike sentensi zinazojumuisha vizuri na vibaya.
MASWALI DADISI
- Unatumia maneno yapi kuelezea vile mtu alivyofanya jambo?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika shughuli za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Uhusiano na masuala mtambuko: uraia – haki za watoto -wanafunzi wanahamasishwa kuhusu haki zake.
Uhusiano na Masomo mengine: Environmental Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- nyimbo na mashairi kuhusu haki za watoto.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji haki za kijamii heshima.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuwahamasisha wengine katika jamii kuhusu haki za watoto.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuuliza maswali kuhusu haki za watoto
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia vizuri na vibaya katika sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema na kwa ukakamavu
- anatambua haki za watoto na kuzitilia maanani katika mawasiliano
- anatumia msamiati wa haki za watoto kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha
- anatetea haki za watoto kwa ukakamavu
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa ubunifu na usahihi
- anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo na kwa ubunifu wa hali ya juu.
- anaandika kwa hati nadhifu.
Kufikia Matarajio
- Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anatambua haki za watoto
- anatumia msamiati wa haki za watoto ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anatetea haki za watoto
- anajibu maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- anatumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anatambua haki za watoto
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anajibu baadhi ya maswali ya ufahamu katika hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto kiasi katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
- Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutambua haki za watoto
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa haki za watoto kwenye sentensi
- ana changamoto katika kusoma kazi anazopewa
- ana changamoto katika kujibu maswali ya ufahamu kwenye hadithi na masimulizi kwa usahihi
- ana changamoto katika kutumia vivumishi vizuri na vibaya kutunga sentensi ifaavyo
- ana changamoto katika kusoma.