MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua picha za vyombo mbalimbali vya usafiri ili
kuimarisha ufahamu wa hadithi,
- kuelezea maana ya maneno yaliyotumiwa katika hadithi ili
kuimarisha ufahamu wa
hadithi,
- kusikiliza hadithi inaposomwa na mwalimu ili kuimarisha umakinifu,
- kusoma hadithi zinazohusu usafiri ili kujenga stadi ya kusoma,
- kufahamu hadithi aliyoisoma kuhusu usafiri ili kupata ujumbe unaodhamiriwa,
- kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku ili kukuza ari ya usomaji huru.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
- Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza mwalimu anaposoma hadithi kisha asome na mwalimu na baadaye asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
- Mwanafunzi asimulie hadithi aliyoisoma au kusomewa kwa kutumia maneno yake mwenyewe.
- Mwanafunzi aweza kurekodiwa akisoma vizuri kwa video au kinasasauti ili wanafunzi waweze kutazama na kusikiliza jinsi ya kusoma hadithi kwa ufasaha.
- Mwanafunzi aweza kufanya ziara ya kwenda kuona vyombo vya usafiri kwenye vituo vya vyombo mbalimbali vya usafiri.
- Mwanafunzi ajibu maswali ya ufahamu akiwa peke yake, wawili wawili au katika vikundi.
MASWALI DADISI
- Umewahi kusoma hadithi ipi?
- Ni hadithi ipi iliyokufurahisha zaidi?
- Unamkumbuka mhusika gani katika hadithi uliyosoma?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika kazi za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kujifunza: mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kutumia vipengee vilivyofunzwa vya sarufi kwenye mawasiliano ubunifu – mwanafunzi anatumia ubunifu katika kutunga sentensi na masimulizi.
Uhusiano na masuala Mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu- usalama katika usafiri –wanashughulikia vyombo vya usafiri.
Uhusiano na Masomo Mengine:
Environmental Activities na English Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- mashairi na nyimbo kuhusu usafiri
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji heshima.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuwahamasisha wengine kuhusu usalama barabarani.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuuliza maswali kuhusu vyombo vya usafiri
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia herufi kubwa kuakifisha maneno na sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anataja majina ya vyombo vya usafiri kwa wepesi
- anatumia msamiati wa usafiri kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha.
- anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma na kusomewa
- anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi kwa wakati
- anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja majina ya vyombo vya
usafiri
- anatumia msamiati wa usafiri ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anafahamu hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma na kusomewa
- anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anataja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa usafiri kwenye sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anafahamu baadhi ya hadithi alizosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto kiasi katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutaja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa usafiri kwenye sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
ana changamoto katika kuandika.