Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

a) kutambua kwa kutaja vyombo mbalimbali vya usafiri ili kuimarisha mawasiliano,

  • kuzungumza kuhusu vyombo vya usafiri ili kuimarisha uwezo wa kujieleza,
  • kusikiliza visa kuhusu usafiri ili kuimarisha umakinifu na ukakamavu katika kujieleza,
  • kufurahia masimulizi kuhusu vyombo vya usafiri ili kuimarisha mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

• Mwanafunzi atambue aina mbalimbali za vyombo vya usafiri k.v. matatu, basi, lori, pikipiki, garimoshi, gari dogo, ndege na meli kwa kutumia picha au vyombo vya kiteknolojia.

  • Mwanafunzi asimulie kuhusu vyombo vya usafiri, kwa mfano; Mimi nilisafiri kwa matatu.
  • Mwanafunzi ashiriki katika mjadala darasani au katika vikundi kuhusu vyombo mbalimbali vya usafiri.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza masimulizi kuhusu vyombo vya usafiri kwa kutumia video au kinasa sauti.

MASWALI DADISI

  1. Je, ni safari gani

umewahi kufanya?

  • Je, unasafiria vyombo  gani?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika kazi za vikundi  ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kujifunza: mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kutumia vipengee vilivyofunzwa vya sarufi kwenye mawasiliano ubunifu – mwanafunzi anatumia ubunifu katika kutunga sentensi na masimulizi.

Uhusiano na masuala Mtambuko: 

elimu ya maendeleo endelevu- usalama katika usafiri –wanashughulikia vyombo vya usafiri.  

Uhusiano na Masomo Mengine: 

Environmental Activities na English Activities                                                                               

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

  • kazi ya vikundi 
  • michezo
  • mashairi na nyimbo kuhusu usafiri 

 Uhusiano na Maadili:  

uwajibikaji  heshima.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji:  kuwahamasisha wengine kuhusu usalama barabarani.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
  • kuuliza maswali kuhusu vyombo vya usafiri 
  • kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa 
  • kuchunguza jinsi anavyotumia herufi kubwa kuakifisha maneno na sentensi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
  • anataja majina ya vyombo vya usafiri kwa wepesi 
  • anatumia msamiati wa usafiri kwa ubunifu katika sentensi
  • anasoma kwa ufasaha.
  • anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma na kusomewa
  • anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi kwa wakati
  • anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti lengwa vyema
  • anataja majina ya vyombo vya

usafiri 

  • anatumia msamiati wa usafiri ifaavyo katika sentensi
  • anasoma ifaavyo
  • anafahamu hadithi aliyosimuliwa,  aliyosoma na kusomewa
  • anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi
  • anaandika kwa hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
  • anataja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri 
  • ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa usafiri kwenye sentensi
  • anasoma baadhi ya kazi anazopewa
  • anafahamu  baadhi ya hadithi alizosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
  • ana changamoto kiasi katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
  • anaandika kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti lengwa 
  • ana changamoto katika kutaja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri 
  • ana changamoto katika kutumia msamiati wa usafiri kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kusoma
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
  • ana changamoto  katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
  • ana changamoto katika kuandika.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *