MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri katika kuimarisha mawasiliano,
- kusoma majina ya vyombo vya usafiri na msamiati mwingine wa usafiri katika sentensi ili kuimarisha usomaji bora,
- kutumia msamiati wa usafiri kutungia sentensi katika kuimarisha stadi ya kuzungumza na kuandika,
- kuandika majina ya vyombo vya usafiri na msamiati mwingine wa usafiri ili kuimarisha stadi ya kuandika,
- kuthamini vyombo vya usafiri katika maisha ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati wa vyombo vya usafiri k.v. matatu, basi, lori, pikipiki, garimoshi, gari dogo, ndege na meli.
- Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaohusu usafiri.
- Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha zinazolenga usafiri.
- Mwanafunzi achore baadhi ya vyombo vya usafiri na kuvitambua kwa majina.
- Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu shughuli za usafiri.
- Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa vyombo vya usafiri.
MASWALI DADISI
- Umewahi kutumia chombo kipi cha kusafiria?
- Unajua vyombo gani vingine vya usafiri?
- Je, ni maneno gani yanayotumiwa usafiri?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – wanafunzi wanashiriki katika kazi za vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kujifunza: mwanafunzi atapata hamu ya kutaka kutumia vipengee vilivyofunzwa vya sarufi kwenye mawasiliano ubunifu – mwanafunzi anatumia ubunifu katika kutunga sentensi na masimulizi.
Uhusiano na masuala Mtambuko:
elimu ya maendeleo endelevu- usalama katika usafiri –wanashughulikia vyombo vya usafiri.
Uhusiano na Masomo Mengine:
Environmental Activities na English Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
- kazi ya vikundi
- michezo
- mashairi na nyimbo kuhusu usafiri
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji heshima.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuwahamasisha wengine kuhusu usalama barabarani.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotamka sauti zilizofunzwa
- kuuliza maswali kuhusu vyombo vya usafiri
- kuchunguza jinsi mwanafunzi anavyojibu maswali ya masimulizi na hadithi na kutoa muhtasari wa hadithi aliyosomewa au kusimuliwa
- kuchunguza jinsi anavyotumia herufi kubwa kuakifisha maneno na sentensi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa kwa ufasaha
- anataja majina ya vyombo vya usafiri kwa wepesi
- anatumia msamiati wa usafiri kwa ubunifu katika sentensi
- anasoma kwa ufasaha.
- anafahamu kwa urahisi hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma na kusomewa
- anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi kwa wakati
- anaandika kwa hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti lengwa vyema
- anataja majina ya vyombo vya
usafiri
- anatumia msamiati wa usafiri ifaavyo katika sentensi
- anasoma ifaavyo
- anafahamu hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma na kusomewa
- anatumia herufi kubwa ipasavyo katika kuakifisha maneno na sentensi
- anaandika kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka baadhi ya sauti lengwa vyema
- anataja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri
- ana changamoto katika kutumia baadhi ya msamiati wa usafiri kwenye sentensi
- anasoma baadhi ya kazi anazopewa
- anafahamu baadhi ya hadithi alizosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto kiasi katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
- anaandika kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti lengwa
- ana changamoto katika kutaja baadhi ya majina ya vyombo vya usafiri
- ana changamoto katika kutumia msamiati wa usafiri kwenye sentensi
- ana changamoto katika kusoma
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosimuliwa, aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto katika kuakifisha maneno na sentensi kwa kutumia herufi kubwa
- ana changamoto katika kuandika.