MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua msamiati wa kazi mbalimbali ili kuimarisha mawasiliano,
- kutunga sentensi akitumia msamiati wa kazi mbalimbali ili kujenga ubunifu,
- kusoma maneno na sentensi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha usomaji,
- kuandika maneno na sentensi kuhusu kazi mbalimbali ili kuimarisha uandishi,
- kuthamini kazi mbalimbali ili kutambua huduma zinazotolea na watu wanaofanya kazi mbalimbali.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi atazame picha, michoro au DVD inayoonyesha watu na kazi mbalimbali k.v ualimu, ukulima, udaktari, uyaya, unesi na ubawabu na kuzitambua peke yake au katika vikundi.
- Wanafunzi waweza kuambatanisha kadi za maneno na kazi mbalimbali wakiwa katika vikundi.
- Mwanafunzi aeleze kazi mbalimbali.
- Mwanafunzi aandike majina ya kazi mbalimbali.
- Mwanafunzi asome msamiati wa kazi mbalimbali katika kadi, chati n.k.
- Mwanafunzi aandike sentensi kuhusu kazi mbalimbali.
- Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi akitumia msamiati wa kazi mbalimbali.
MASWALI DADISI
- Ni neno gani unaloweza kusoma kwenye kadi?
- Ni kazi ipi unayoipenda?
- Kwa nini watu hufanya kazi?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana kufanya kazi katika vikundi
kujiamini/kujithamini – kuthamini na kutambua kazi mbalimbali; Kujibu maswali ya kisarufi vilivyo ubunifu – Katika utunzi wa sentensi na kujibu maswali ya ufahamu ambayo majibu yake si ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Uhusiano na masuala mtambuko:
shughuli zinazomsaidia mwanafunzi: mwongozo wa ajira – kuthamini kazi mbalimbali
Uhusiano na masomo mengine: Engilish Activities na Environmental Activities
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji; uzalendo; umoja na heshima
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia wazazi katika kazi za nyumbani na katika jamii kuthamini kazi zinazofanywa na wazazi, ndugu na watu wengine katika jamii.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
kushiriki katika maigizo yanayohusu kazi mbalimbali kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu kazi mbalimbali katika tamasha za muziki
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
- kuchunguza anavyotambua kazi mbalimbali
- kuchunguza anavyotumia ukanusho wa nyakati katika mawasiliano
- kuchunguza anavyosoma na kusimulia hadithi
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
- anaelezea kuhusu kazi mbalimbali kwa ufasaha.
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia kikomo ipasavyo
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo.
- anaelezea kuhusu kazi mbalimbali
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anatumia kikomo ipasavyo
- anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatamka sauti ipasavyo
- anataja kazi mbalimbali
- anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi vilivyo
- anafahamu baadhi ya hadithi alizosoma au kusomewa.
- anatumia kikomo
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kutamka sauti
- ana changamoto katika kuelezea kazi mbalimbali
- ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi
- anachangamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
- ana changamoto katika kutumia kikomo
- ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyopewa.