Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora,
  2. kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora,
  3. kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji,
  4. kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti, lengwa ili kuimarisha usomaji
  5. kusoma kwa sauti hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kuimarisha matamshi na usomaji, 
  6. kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora,
  7. kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi bora,
  8. kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi atambue sauti py na vy katika maneno
  • Mwanafunzi amsikilize mwalimu akitamka silabi zinazotokana na sauti lengwa kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa  pekee, wawili na  darasa zima k.m pya, pye, vya na vye.
  • Mwanafunzi aweza  kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi, projekta na kipasasauti ili kuimarisha matamshi yake.
  • Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
  •  Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno kwa mfano k. m mpya, kipya, kompyuta, vyema, vyoo na vyote.
  • Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa. 
  • Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kuyagawa yaliyo marefu zaidi katika sehemu ndogo ndogo.
  • Wanafunzi waweza  kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa darasani au wawili wawili. 
  • Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yaliyo na herufi za sauti lengwa na kuyaandika.

MASWALI DADISI

  1. Je, ni sauti zipi unazojua kutamka?
  2. Je, ni sauti zipi zinazokutatiza kutamka?
  3. Je, ni sauti zipi unazotamka bila shida?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana kufanya kazi katika vikundi

kujiamini/kujithamini – kuthamini na kutambua kazi mbalimbali; Kujibu maswali ya kisarufi vilivyo ubunifu – Katika utunzi wa sentensi na kujibu maswali ya ufahamu ambayo majibu yake si ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

shughuli zinazomsaidia mwanafunzi: mwongozo wa ajira – kuthamini kazi mbalimbali

Uhusiano na masomo mengine: Engilish Activities na Environmental Activities

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji; uzalendo; umoja na heshima

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia wazazi katika kazi za nyumbani na katika jamii kuthamini kazi zinazofanywa na wazazi, ndugu na watu wengine katika jamii.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo yanayohusu kazi mbalimbali kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu kazi mbalimbali katika tamasha za muziki

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotambua kazi mbalimbali 
  • kuchunguza anavyotumia ukanusho wa nyakati katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyosoma na kusimulia hadithi 
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
  • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali kwa ufasaha.
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia kikomo ipasavyo
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo.
  • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali 
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha 
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia kikomo ipasavyo
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anataja kazi mbalimbali
  • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi  vilivyo
  • anafahamu baadhi ya hadithi alizosoma au kusomewa.
  • anatumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka sauti 
  • ana changamoto katika kuelezea kazi mbalimbali
  • ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi 
  • anachangamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa 
  • ana changamoto katika kutumia kikomo 
  • ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyopewa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *