Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua ukanusho wa -li-; na-; -ta- katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano,
 2. kusoma ukanusho wa nyakati katika sentensi ili kuimarisha usomaji,
 3. kuandika ukanusho wa nyakati katika sentensi ili kujenga ubunifu,
 4. kuchangamkia matumizi ya nyakati katika mawasiliano.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

 • Wanafunzi watumie -li-; -na-; -ta- kuelezea vitendo walivyofanya katika wakati uliopita (LI), ulipo (NA) na ujao (TA) wakiwa katika vikundi au wawili wawili.
 • Mwanafunzi akamilishe vifungu kwa kutumia -li-; na-; -ta- na ukanusho wake.                     
 • Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi -li-; na-; -ta- na ukanusho wake.
 • Mwanafunzi aweza kupewa zoezi la ukanusho wa nyakati akiwa peke yake, wawili wawili au katika kikundi.
 • Mwanafunzi aweza kutazama jinsi nyakati zinavyokanushwa katika vifaa vya kiteknolojia na kufanyia zoezi kwenye mtandao.

MASWALI DADISI

 1. Unafanya nini sasa?
 2. Ulifanya nini jana?
 3. Utafanya nini kesho?
 4. Je, ni nyakati zipi ambazo unajua kukanusha?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana kufanya kazi katika vikundi

kujiamini/kujithamini – kuthamini na kutambua kazi mbalimbali; Kujibu maswali ya kisarufi vilivyo ubunifu – Katika utunzi wa sentensi na kujibu maswali ya ufahamu ambayo majibu yake si ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

shughuli zinazomsaidia mwanafunzi: mwongozo wa ajira – kuthamini kazi mbalimbali

Uhusiano na masomo mengine: Engilish Activities na Environmental Activities

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji; uzalendo; umoja na heshima

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia wazazi katika kazi za nyumbani na katika jamii kuthamini kazi zinazofanywa na wazazi, ndugu na watu wengine katika jamii.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo yanayohusu kazi mbalimbali kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu kazi mbalimbali katika tamasha za muziki

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
 • kuchunguza anavyotambua kazi mbalimbali 
 • kuchunguza anavyotumia ukanusho wa nyakati katika mawasiliano
 • kuchunguza anavyosoma na kusimulia hadithi 
 • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
 • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali kwa ufasaha.
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatumia kikomo ipasavyo
 • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, hati nadhifu na kwa kasi ifaayo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo.
 • anaelezea kuhusu kazi mbalimbali 
 • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha 
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anatumia kikomo ipasavyo
 • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anatamka sauti ipasavyo
 • anataja kazi mbalimbali
 • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi  vilivyo
 • anafahamu baadhi ya hadithi alizosoma au kusomewa.
 • anatumia kikomo 
 • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kutamka sauti 
 • ana changamoto katika kuelezea kazi mbalimbali
 • ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi 
 • anachangamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa 
 • ana changamoto katika kutumia kikomo 

ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyopewa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *