Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua msamiati ambao hutumiwa katika usalama ili kuimarisha mawasiliano,
  2. kusoma msamiati unaohusiana na usalama ili kujenga usomaji bora,
  3. kueleza maana ya msamiati wa usalama ili kuimarisha ufahamu,
  4. kutumia msamiati wa usalama katika sentensi ili kuimarisha ufahamu,
  5. kuandika maneno yanayohusiana na usalama ili kujenga uandishi bora,
  6. kuthamini usalama katika mazingira yake.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na usalama kwa kutumia kadi za maneno.
  • Mwanafunzi aeleze maana ya msamiati wa usalama akiwa peke yake au katika vikundi.
  • Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa usalama.
  • Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu usalama

k.m. utekaji nyara na moto na kisha kujadili jinsi ya kujilinda kutokana na hatari.

  • Mwanafunzi atazame michoro na picha zinazolenga maana ya maneno yanayohusiana na usalama.
  • Wanafunzi wajadiliane kuhusu umuhimu wa usalama.

MASWALI DADISI

  1. Je, ni nini maana ya usalama?
  2. Usalama huhusisha mambo yapi?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya usalama – kupitia kwa kutambua umuhimu na mbinu za kujilinda na hali zinazohatarisha usalama

Stadi za maisha – mbinu za kujilinda dhidi ya tisho kwa usalama wake.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities; Hygiene and Nutrition na English Activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usalama katika tamasha mbalimbali.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji -kuwa na msimamo thabiti katika uamuzi wake haki za kijamii- kufuata haki zake anapodhulumiwa.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia kuhamasisha jamii kuhusu usalama kushiriki katika kutetea haki za kijamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa usalama katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia vinyume vya vitendo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
  • kufuatilia mwandiko wake.
  •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua na kutumia mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
  • anatumia maneno ya maagano
  • ifaavyo kila wakati
  • anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ubunifu na ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha na ukakamavu
  •  anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
  •  anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo. 

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
  • anatumia maneno ya maagano ifaavyo
  • anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha
  • anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora. 

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

•             anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake

•             anatumia maneno ya maagano ifaavyo

•             anaelezea kuhusu kisa alichoshuhudia bila mtiririko wenye mantiki

•             anasoma maneno, sentensi na baadhi ya hadithi  kwa ufasaha

 •            ana changamoto katika kuandika vinyume vya baadhi ya vitendo kwa usahihi

•             anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

•             ana changamoto katika kutambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake

•             ana changamoto katika kutumia baadhi ya maneno ya maagano kwenye mawasiliano

•             ana changamoto katika kusimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama

•             ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha

•             ana changamoto katika kuandika vinyume vya vitendo kwa usahihi

•             ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *