Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua maneno yanayotumiwa katika maagano ili kuwezesha mazungumzo,
  2. kutumia maneno yanayotumiwa katika maagano kwenye mawasiliano,
  3. kujibu maagano kwa njia ifaayo ili kudhihirisha ufahamu,
  4. kuthamini matumizi ya maagano katika mawasiliano ya kila siku.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi anaweza kueleza matumizi ya maagano kama vile: kwaheri; siku njema, mchana mwema, safiri salama na usiku mwema.
  • Mwanafunzi atazame michoro inayoashiria vitendo vya kuagana.
  • Mwanafunzi ashiriki katika maigizo ya kuagana.
  • Mwanafunzi aweza kutazama vibonzo katika tarakilishi vikiigiza vitendo na maneno mbalimbali ya kuagana.
  • Mwanafunzi aweza kutaja neno la kuagana linalofaa kutokana na maelezo mbalimbali akiwa peke yake, wawili wawili au katika vikundi.

MASWALI DADISI

  1. Je, ulipoagana na mzazi asubuhi alikwambiaje?
  2. Je, mzazi hukwambiaje unapoenda kulala?
  3. Mtu anaposafiri anaambiwaje?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya usalama – kupitia kwa kutambua umuhimu na mbinu za kujilinda na hali zinazohatarisha usalama

Stadi za maisha – mbinu za kujilinda dhidi ya tisho kwa usalama wake.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities; Hygiene and Nutrition na English Activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usalama katika tamasha mbalimbali.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji -kuwa na msimamo thabiti katika uamuzi wake haki za kijamii- kufuata haki zake anapodhulumiwa.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia kuhamasisha jamii kuhusu usalama kushiriki katika kutetea haki za kijamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa usalama katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia vinyume vya vitendo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
  • kufuatilia mwandiko wake.
  •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua na kutumia mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
  • anatumia maneno ya maagano
  • ifaavyo kila wakati
  • anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ubunifu na ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha na ukakamavu
  •  anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
  •  anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo. 

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
  • anatumia maneno ya maagano ifaavyo
  • anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha
  • anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora. 

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

•             anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake

•             anatumia maneno ya maagano ifaavyo

•             anaelezea kuhusu kisa alichoshuhudia bila mtiririko wenye mantiki

•             anasoma maneno, sentensi na baadhi ya hadithi  kwa ufasaha

 •            ana changamoto katika kuandika vinyume vya baadhi ya vitendo kwa usahihi

•             anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

•             ana changamoto katika kutambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake

•             ana changamoto katika kutumia baadhi ya maneno ya maagano kwenye mawasiliano

•             ana changamoto katika kusimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama

•             ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi  kwa ufasaha

•             ana changamoto katika kuandika vinyume vya vitendo kwa usahihi

•             ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *