MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua picha zinazoonyesha usalama katika mazingira mbalimbali ili kurahisisha ufahamu,
- kutambua maneno yanayohusiana na usalama ili kuyatumia katika mawasiliano,
- kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu usalama ili kuimarisha ufahamu,
- kusoma hadithi kuhusu usalama ili kujenga usikivu,
- kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu usalama ili kupata ujumbe,
- kuthamini umuhimu wa usalama katika maisha ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
- Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi
- Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
- Mwanafunzi ashiriki kusoma kama darasa, wakiwa wawili wawili na baadaye asome peke yake.
- Wanafunzi wasomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi.
- Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kinasasauti.
- Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu mzima au mtoto akisoma hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomi huo
- Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
- Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu usalama.
- Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
- Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kutokana na hadithi.
MASWALI DADISI
- Je, usalama unahusu nini?
- Ukosefu wa salama husababishwa na nini?
- Unapokosa usalama unafaa kufanya nini?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya usalama – kupitia kwa kutambua umuhimu na mbinu za kujilinda na hali zinazohatarisha usalama
Stadi za maisha – mbinu za kujilinda dhidi ya tisho kwa usalama wake.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities; Hygiene and Nutrition na English Activities.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usalama katika tamasha mbalimbali.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji -kuwa na msimamo thabiti katika uamuzi wake haki za kijamii- kufuata haki zake anapodhulumiwa.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia kuhamasisha jamii kuhusu usalama kushiriki katika kutetea haki za kijamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa usalama katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia vinyume vya vitendo katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano
- ifaavyo kila wakati
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ubunifu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano ifaavyo
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
• anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• anatumia maneno ya maagano ifaavyo
• anaelezea kuhusu kisa alichoshuhudia bila mtiririko wenye mantiki
• anasoma maneno, sentensi na baadhi ya hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya baadhi ya vitendo kwa usahihi
• anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
• ana changamoto katika kutambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• ana changamoto katika kutumia baadhi ya maneno ya maagano kwenye mawasiliano
• ana changamoto katika kusimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama
• ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
• ana changamoto katika kuandika kisa.