MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua kisa chenye mtiririko,
- kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada,
- kufurahia uandishi wa visa tofauti maishani.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aweza kupewa hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
- Mwanafunzi aongozwe kujadili yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.
- Mwanafunzi aweza kusoma kielelezo cha kisa kilichoandikwa.
- Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
- Mwanafunzi apewe fursa ya kuandika kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji.
MASWALI DADISI
- Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa?
- Je, unaweza kuandika kisa gani kifupi kinachohusiana na usalama?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya usalama – kupitia kwa kutambua umuhimu na mbinu za kujilinda na hali zinazohatarisha usalama
Stadi za maisha – mbinu za kujilinda dhidi ya tisho kwa usalama wake.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities; Hygiene and Nutrition na English Activities.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usalama katika tamasha mbalimbali.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji -kuwa na msimamo thabiti katika uamuzi wake haki za kijamii- kufuata haki zake anapodhulumiwa.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia kuhamasisha jamii kuhusu usalama kushiriki katika kutetea haki za kijamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa usalama katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia vinyume vya vitendo katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano
- ifaavyo kila wakati
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ubunifu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano ifaavyo
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
• anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• anatumia maneno ya maagano ifaavyo
• anaelezea kuhusu kisa alichoshuhudia bila mtiririko wenye mantiki
• anasoma maneno, sentensi na baadhi ya hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya baadhi ya vitendo kwa usahihi
• anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
• ana changamoto katika kutambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• ana changamoto katika kutumia baadhi ya maneno ya maagano kwenye mawasiliano
• ana changamoto katika kusimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama
• ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya vitendo kwa usahihi • ana changamoto katika kuandika kisa.