MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutaja vinyume vya vitendo,
- kusoma sentensi zilizo na vinyume vya vitendo,
- kuandika vinyume vya vitendo,
- kuchangamkia kutumia vitendo na vinyume vyake katika mawasiliano ya kila siku.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aweza kufafanuliwa juu ya vinyume vya vitendo kama vile lala-amka; keti- simama; cheka-lia; tabasamu – nuna; nenda-rudi; panda – shuka n.k.
- Wanafunzi waweza kuigiza vinyume vya vitendo wakiwa wawili wawili.
- Mwanafunzi aweza kushirikishwa kutunga na kusoma sentensi zilizo na vinyume vya vitendo.
- Mwanafunzi aweza kuelekezwa kuandika vinyume vya vitendo.
MASWALI DADISI
1) Je, unajua vinyume vya vitendo unavyofanya kila siku?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya usalama – kupitia kwa kutambua umuhimu na mbinu za kujilinda na hali zinazohatarisha usalama
Stadi za maisha – mbinu za kujilinda dhidi ya tisho kwa usalama wake.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities; Hygiene and Nutrition na English Activities.
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kushiriki katika kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usalama katika tamasha mbalimbali.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji -kuwa na msimamo thabiti katika uamuzi wake haki za kijamii- kufuata haki zake anapodhulumiwa.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kusaidia kuhamasisha jamii kuhusu usalama kushiriki katika kutetea haki za kijamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa usalama katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia vinyume vya vitendo katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua na kutumia mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano
- ifaavyo kila wakati
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ubunifu na ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
- anatumia maneno ya maagano ifaavyo
- anasimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama kwa ufasaha
- anasoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
- anaandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
- anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
• anatambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• anatumia maneno ya maagano ifaavyo
• anaelezea kuhusu kisa alichoshuhudia bila mtiririko wenye mantiki
• anasoma maneno, sentensi na baadhi ya hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya baadhi ya vitendo kwa usahihi
• anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
• ana changamoto katika kutambua mbinu mbalimbali za kujiepusha na hali zinazoweza kuhatarisha usalama wake
• ana changamoto katika kutumia baadhi ya maneno ya maagano kwenye mawasiliano
• ana changamoto katika kusimulia kisa alichokishuhudia kuhusu usalama
• ana changamoto katika kusoma maneno, sentensi na hadithi kwa ufasaha
• ana changamoto katika kuandika vinyume vya vitendo kwa usahihi
• ana changamoto katika kuandika kisa.