Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua msamiati wa usafi wa mazingira, 
  2. kutumia msamiati wa usafi wa mazingira katika sentensi, 
  3. kubainisha mazingira safi na yale machafu, 
  4. kuthamini mazingira safi.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi aweza kuelekezwa kusoma maneno yanayohusiana na usalama kwa kutumia kadi za maneno.
  • Mwanafunzi aweza kuelekezwa kutoa maana ya msamiati unaohusiana na usafi wa mazingira.
  • Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu maana za maneno yanayohusiana na usafi wa mazingira.
  • Mwanafunzi aweza  kutunga sentensi sahihi kwa kutumia msamiati unaohusiana na usafi wa mazingira.
  • Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu usafi wa mazingira k.m. kuokota na kuchoma taka, kufyeka nyasi n.k.
  • Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha zinazolenga maana za maneno kuhusu usafi wa mazingira.
  • Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira wakiwa kwenye vikundi. 

MASWALI DADISI

  1. Je, unajua msamiati gani unaohusiana na usafi wa mazingira?
  2. Unaweza kutumia msamiati gani unaohusiana na usafi wa mazingira katika sentensi?
  3. Mazingira safi ni yapi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendelea kujifunza –  kutambua umuhimu wa mazingira.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu– kupitia kwa kutambua umuhimu wa kudumisha usafi katika mazingira yake.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Hygiene na Nutrition Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

Kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usafi wa mazingira katika tamasha mbalimbali shuleni.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji katika kuweka mazingira yakiwa safi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kusafisha mazingira k.m kuokota taka

Kuwahamasisha wengine kuhusu umuhimu wa kuweka mazingira yakiwa safi.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa usafi wa mazingira katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia haraka na polepole katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
  • kufuatilia mwandiko wake.
  •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ubunifu
  • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu  kwa wepesi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia haraka na polepole kwa usahihi kila wakati
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaavyo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
  • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
  • anafahamu  aliyosoma na kusomewa
  • anatumia haraka na polepole kwa usahihi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
  • anasoma baadhi ya hadithi vilivyo
  • anafahamu  baadhi ya hadithi alizosoma na kusomewa 
  • anatumia haraka na polepole kwa wastani
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kusikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
  • ana changamoto katika kusoma hadithi
  • ana changamoto katika kufahamu aliyosoma na kusomewa 
  • ana changamoto katika kutumia haraka na polepole kwenye sentensi
  • ana changamoto katika kuandika kisa. 

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *