Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutofautisha mazingira safi na yasiyo safi,  
 2. kutambua umuhimu wa mazingira safi, 
 3. kusikiliza masimulizi kuhusu usafi wa mazingira, 
 4. kuelezea kuhusu usafi wa mazingira, 
 5. kuelezea jinsi ya kutunza mazingira yake, 
 6. kufurahia mazingira safi maishani mwake.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

 • Mwanafunzi aelezee maana ya usafi wa mazingira.
 • Wanafunzi waongozwe katika vikundi kusimulia  visa vinavyohusiana na usafi wa mazingira k.v. umuhimu na jinsi ya kutunza mazingira.
 • Mwanafunzi aigize jinsi ya kudumisha usafi katika mazingira yake.
 • Wanafunzi waweza kutazama video inayohusu mazingira safi na chafu kisha wabainishe mazingira wanayofurahia.
 • Mwanafunzi anaweza kuchora vifaa vinavyotumiwa kusafisha mazingira. 
 • Wanafunzi waweza kujadiliana kuhusu jinsi wanavyoweza kuchangia katika usafi wa mazingira.
 • Mgeni aweza kualikwa ili kusimulia kuhusu mazingira huku wanafunzi wakiandika yaliyo muhimu pamoja na kuuliza na kujibu maswali.

MASWALI DADISI

 1. Ni nini maana ya mazingira?
 2. Mazingira safi ni yapi?
 3. Je, tunawezaje kuboresha mazingira?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendelea kujifunza –  kutambua umuhimu wa mazingira.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu– kupitia kwa kutambua umuhimu wa kudumisha usafi katika mazingira yake.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Hygiene na Nutrition Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

Kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usafi wa mazingira katika tamasha mbalimbali shuleni.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji katika kuweka mazingira yakiwa safi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kusafisha mazingira k.m kuokota taka

Kuwahamasisha wengine kuhusu umuhimu wa kuweka mazingira yakiwa safi.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa usafi wa mazingira katika mawasiliano 
 • kuchunguza anavyotumia haraka na polepole katika mawasiliano
 • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
 • kufuatilia mwandiko wake.
 •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ubunifu
 • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu  kwa wepesi aliyosoma na kusomewa
 • anatumia haraka na polepole kwa usahihi kila wakati
 • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaavyo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
 • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
 • anafahamu  aliyosoma na kusomewa
 • anatumia haraka na polepole kwa usahihi
 • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

 • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
 • anasoma baadhi ya hadithi vilivyo
 • anafahamu  baadhi ya hadithi alizosoma na kusomewa 
 • anatumia haraka na polepole kwa wastani
 • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

 • ana changamoto katika kusikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
 • ana changamoto katika kusoma hadithi
 • ana changamoto katika kufahamu aliyosoma na kusomewa 
 • ana changamoto katika kutumia haraka na polepole kwenye sentensi

ana changamoto katika kuandika kisa. 

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

One thought on “CBC Grade 3-Curriculum Designs-kazi ya Kiswahili-6.0-USAFI WA MAZINGIRA-mada ndogo-6.2-Kusikiliza na Kuzungumza: Masimulizi”
 1. Thank you very much for sharing. Your article was very helpful for me to build a paper on gate.io. After reading your article, I think the idea is very good and the creative techniques are also very innovative. However, I have some different opinions, and I will continue to follow your reply.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *