Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua msamiati uliotumiwa katika hadithi, 
  2. kusikiliza mwalimu kwa makini anaposoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira, 
  3. kusoma hadithi kuhusu mazingira safi, 
  4. kufahamu hadithi aliyosoma na aliyosomewa kuhusu usafi wa mazingira, 
  5. kuthamini mazingira safi. 

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi aweza  kujadili kuhusu picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi aweza  kutabiri kitakachotokea kwenye hadithi.
  • Mwanafunzi aweza  kuthibitisha utabiri wake baada ya kusoma hadithi.
  • Mwanafunzi aweza  kufahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.
  • Wanafunzi waweza kusoma kama darasa, wakiwa wawili na baadaye asome peke yake.
  • Mwanafunzi aweza  kutoa muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.
  • Mwanafunzi atabiri kitakachotokea katika hadithi 
  • Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili.
  • Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi husika ikisomwa kupitia kinasasauti.
  • Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi husika kwa ufasaha, kisha aige usomi ule.
  • Wanafunzi waweza kusomeana hadithi katika vikundi.
  • Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu mazingira.
  • Mwanafunzi aulize na kujibu maswali kudhihirisha ufahamu.

MASWALI DADISI

  1. Je, unaweza kukumbuka hadithi gani uliyosoma?
  2. Je, hadithi

unayoweza kukumbuka inahusu nini?

  • Je, umeweza kusoma hadithi ngapi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendelea kujifunza –  kutambua umuhimu wa mazingira.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu– kupitia kwa kutambua umuhimu wa kudumisha usafi katika mazingira yake.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Hygiene na Nutrition Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

Kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usafi wa mazingira katika tamasha mbalimbali shuleni.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji katika kuweka mazingira yakiwa safi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kusafisha mazingira k.m kuokota taka

Kuwahamasisha wengine kuhusu umuhimu wa kuweka mazingira yakiwa safi.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa usafi wa mazingira katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia haraka na polepole katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
  • kufuatilia mwandiko wake.
  •  

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ubunifu
  • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu  kwa wepesi aliyosoma na kusomewa
  • anatumia haraka na polepole kwa usahihi kila wakati
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaavyo. 

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
  • anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
  • anafahamu  aliyosoma na kusomewa
  • anatumia haraka na polepole kwa usahihi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
  • anasoma baadhi ya hadithi vilivyo
  • anafahamu  baadhi ya hadithi alizosoma na kusomewa 
  • anatumia haraka na polepole kwa wastani
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kusikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
  • ana changamoto katika kusoma hadithi
  • ana changamoto katika kufahamu aliyosoma na kusomewa 
  • ana changamoto katika kutumia haraka na polepole kwenye sentensi

ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *