MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kutambua matumizi ya haraka na polepole ili kuimarisha mawasiliano mwafaka,
- kutumia haraka na polepole katika kutunga sentensi ili
kuimarisha mawasiliano mwafaka,
- kusoma sentensi zilizo na matumizi ya haraka na polepole ili kujenga usomaji bora,
- kuandika majina na sentensi kuhusu ndege ili kuimarisha uandishi bora,
- Kuchangamkia matumizi ya haraka na polepole katika mawasiliano.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia haraka na polepole.
- Mwanafunzi aweza kubainisha matumizi ya vielezi vya jinsi vinavyofunzwa kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia.
- Mwanafunzi atazame vitu mbalimbali na avirejelee kwa kutumia haraka na polepole k.m Mtoto anatembea polepole.
MASWALI DADISI
- Unatumia maneno gani kuelezea namna mtu alivyofanya jambo?
- Unatumia maneno gani kuelezea namna mtu anavyotembea?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza hamu ya kuendelea kujifunza – kutambua umuhimu wa mazingira.
Uhusiano na masuala mtambuko:
Elimu ya maendeleo endelevu– kupitia kwa kutambua umuhimu wa kudumisha usafi katika mazingira yake.
Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Hygiene na Nutrition Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:
Kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu usafi wa mazingira katika tamasha mbalimbali shuleni.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji katika kuweka mazingira yakiwa safi.
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kusafisha mazingira k.m kuokota taka
Kuwahamasisha wengine kuhusu umuhimu wa kuweka mazingira yakiwa safi.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa usafi wa mazingira katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia haraka na polepole katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi
- kufuatilia mwandiko wake.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ubunifu
- anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi aliyosoma na kusomewa
- anatumia haraka na polepole kwa usahihi kila wakati
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaavyo.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
- anasoma hadithi kuhusu usafi wa mazingira kwa ufasaha
- anafahamu aliyosoma na kusomewa
- anatumia haraka na polepole kwa usahihi
- anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi,
- anasikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
- anasoma baadhi ya hadithi vilivyo
- anafahamu baadhi ya hadithi alizosoma na kusomewa
- anatumia haraka na polepole kwa wastani
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi,
- ana changamoto katika kusikiliza na kuzungumza kuhusu usafi wa mazingira
- ana changamoto katika kusoma hadithi
- ana changamoto katika kufahamu aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kutumia haraka na polepole kwenye sentensi
- ana changamoto katika kuandika kisa.