Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua matumizi ya; -ake na – ao ili kuimarisha mawasiliano,
  2. kusoma vifungu vya maneno vinavyojumuisha  -ake na -ao ili kujenga usomaji,
  3. kutunga sentensi akitumia  -ake na -ao ili kuimarisha ubunifu,
  4. kuandika sentensi akitumia -ake na -ao ili kujenga uandishi bora,
  5. kuchangamkia kurejelea vitu vyake na vya wenzake akitumia  -ake na -ao katika mawasiliano ya kila siku.

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi aonyeshe vitu vyake na vya wengine darasani na kuvirejelea akitumia -ake na –ao. 
  • Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi -ake na –ao.
  • Mwananafunzi akamilishe vifungu kwa kutumia  -ake na –ao  km Kalamu _______  (kalamu yake)- Kalamu ______ (Kalamu zao); kitabu  ______ (Kitabu chako) – Kitabu ______(Vitabu vyao).  
  • Mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia –ake na – ao.  
  • Mwanafunzi aweza kutumia tarakilishi kufanya zoezi.  

                MASWALI DADISI

  1. Je, utatumia neno gani kuonyesha kwamba unachozungumzia ni chako?
  2. Je, ni nini wingi wa –ake?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani kufikiri kwa kina na kutatua matatizo – Katika kujibu maswali ya ufahamu yasiyo na majibu ya moja kwa moja ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

uraia: uzalendo – kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa.

Uhusiano na masomo mengine: Environmental Activities na Movement and Creative Activities.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika uskauti shuleni kupandisha bendera shuleni kushiriki katika kuimba wimbo wa taifa kuimba na kukariri mashairi kuhusu uzalendo. 

Uhusiano na Maadili: 

umoja, uzalendo, haki za kijamii, uwajibikaji, mapenzi kwa nchi, heshima na amani.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuimba nyimbo zinazokuza uzalendo katika sherehe mbalimbali.

 Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa shambani katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia –ake na -ao katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake
  • kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo na kwa ufasaha
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatunga sentensi sahihi akitumia – ake na -ao kila wakati
  • anaandika kisa kifupi kwa hati nadhifu, ubunifu, mtiririko mwafaka na kwa haraka. 

Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anatunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • anaandika kisa kifupi kwa hati bora na kwa mtiririko ufaao.

Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia visa vinavyohusiana na uzalendo.
  • anasoma hadithi
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • anajaribu kuandika kisa kifupi kwa hati zinazosomeka.

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutamka  sauti ipasavyo
  • ana changamoto katika kusimulia visa vinavyohusiana na uzalendo
  • ana changamoto katika kusoma hadithi
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kutunga sentensi sahihi akitumia –ake na -ao 
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *