Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora,
  2. kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora,
  3. kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji,
  4. kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha usomaji,
  5. kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia mwanafunzi kutamka sauti husika katika kuimarisha matamshi na usomaji, 
  6. kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora,
  7. kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi bora,
  8. kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano.

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi atambue sauti mb, nj na ng katika maneno.
  • Mwanafunzi amsikilize mwalimu akitamka silabi zinazotokana na sauti lengwa kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa  pekee, wawili na  darasa zima. Mifano ya silabi hizi ni: mba, mbe, mbi, nja, nje, nji, nga, nge na ngi. 
  • Mwanafunzi aweza  kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi, projekta na kipasasautikipasasauti katika kuimarisha matamshi yake.
  • Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa.
  • Mwanafunzi atambue sauti alizosikia katika maneno kwa mfano mbuzi, mbuni, Septemba, Disemba, njugu, ngazi na funga
  • Mwanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa.
  • Mwanafunzi asome maneno kwa kuunganisha silabi na kugawa maneno yaliyo marefu zaidi katika sehemu ndogo ndogo.
  • Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa darasani au wawili wawili. 
  • Mwanafunzi asikilize imla ya maneno yenye silabi za sauti lengwa na kuyaandika.

                MASWALI DADISI

  1.  Ni sauti zipi unazojua kutamka?
  2. Unajua kusoma herufi  zipi?
  3. Unajua kuandika herufi na maneno yapi yanayoundwa kutokana na sauti mbili zinazotamkwa pamoja?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko:  

elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.

Uhusiano na masomo mengine: 

Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali 

Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji  uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake

kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma hadithi 
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti 
  • ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *