Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

 1. kutambua majina ya miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha mawasiliano,
 2. kutaja miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
 3. kusikiliza masimulizi kuhusu miezi ya mwaka ili kujenga usikivu,
 4. kuthamini umuhimu miezi ya mwaka maishani.

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

 • Mwanafunzi ataje miezi ya mwaka. 
 • Mwanafunzi aweza kuelezea mambo yanayofanyika miezi fulani k.v. kufungua shule mwezi wa Januari, kufunga shule mwezi wa Aprili.
 • Mwanafunzi asimulie kuhusu matukio katika miezi mbalimbali k.v. kuzaliwa, shehere za kidini na kitaifa.
 • Mwanafunzi aweza  kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu miezi ya mwaka.
 • Mwanafunzi asome majina ya miezi ya mwaka kupitia kwa vifaa kama kadi za majina.
 • Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu shughuli zinazofanyika katika miezi tofauti.
 • Mwanafunzi amsomee mwenzake au asomee kikundi, majina ya miezi ya mwaka.
 • Wanafunzi waweza kupewa kadi zilizo na matukio mbalimbali ya mwaka waambatanishe na miezi yenyewe katika vikundi.
 • Mwanafunzi aandike majina ya miezi ya mwaka. 
 • Mwanafunzi aweza kufuatanisha majina ya miezi ya mwaka.  

                MASWALI DADISI

 1. Unajua miezi gani ya mwaka?
 2. Je, ulizaliwa mwezi gani?
 3. Mwaka una miezi mingapi?
 4. Ni mwezi upi wa mwaka huwa na sherehe nyingi?

 Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.

Uhusiano na masomo mengine: 

Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali 

Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji  uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

 • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
 • kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
 • kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
 • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
 • kufuatilia mwandiko wake

kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi;

 • anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
 • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
 • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
 • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
 • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi;

 • anatamka sauti ipasavyo
 • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka 
 • anasoma hadithi kwa ufasaha
 • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika sentensi akitumia kikomo 
 • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi;

 • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
 • anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
 • anasoma hadithi 
 • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
 • anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo 
 • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi;

 • anatamka baadhi ya sauti 
 • ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
 • anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
 • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
 • ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
 • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *