Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kusikiliza hadithi ikisomwa na  mwalimu inayojumuisha miezi ili kuimarisha stadi za kusikiliza na kusoma,
  2. kusoma hadithi zinazojumuisha miezi na nambari ili kuimarisha usomaji,
  3. kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu miezi ya mwaka ili kupata ujumbe,
  4. kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku. 

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi asikilize mwalimu akisoma hadithi. 
  • Mwanafunzi asome hadithi peke yake.
  • Wanafunzi wasomeane hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi. 
  •  Mwanafunzi aweza kutazama video ambapo hadithi inasomwa.
  • Mwanafunzi aweza  kusoma hadithi kwa kutumia jitabu lililowekwa mbele ya darasa.
  • Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma.
  • Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa.

                MASWALI DADISI

  1. Je, ni hadithi gani uliofurahia ukisomewa?
  • Je, waweza kukumbuka nini ulichosoma au kusomewa? 

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.

Uhusiano na masomo mengine: 

Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali 

Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji  uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake

kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma hadithi 
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti 
  • ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *