MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-
- kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi,
- kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi.
MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI
- Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka.
- Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi
k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k.
- Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa.
- Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili.
- Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi:
maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji.
MASWALI DADISI
- Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa?
- Je, unaweza kuandika kisa gani kuhusu jambo ulilofanya katika mwezi fulani wa mwaka?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa:
mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Uhusiano na masuala mtambuko:
elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.
Uhusiano na masomo mengine:
Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities
Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji: kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali
Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.
Uhusiano na Maadili:
uwajibikaji uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).
Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.
Mapendekezo ya Tathmini:
- kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
- kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
- kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
- kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
- kufuatilia mwandiko wake
kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.
Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini
Kuzidisha Matarajio
Mwanafunzi;
- anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
- anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
- anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
- anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
- anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.
Kufikia Matarajio
Mwanafunzi;
- anatamka sauti ipasavyo
- anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
- anasoma hadithi kwa ufasaha
- anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika sentensi akitumia kikomo
- anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.
Kukaribia Matarajio
Mwanafunzi;
- anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
- anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
- anasoma hadithi
- anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
- anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo
- anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.
Mbali na Matarajio
Mwanafunzi;
- anatamka baadhi ya sauti
- ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
- anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
- ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
- ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
- ana changamoto katika kuandika kisa.