Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze;

  1. kutambua nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
  2. kusoma nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha usomaji bora,
  3. kuandika nambari 51- 100 kwa maneno ili kuimarisha uandishi bora,

kuchangamkia kutumia nambari 51 – 100 kwa maneno katika mazungumzo yake.

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi asome majina ya nambari 51-100
  • Wanafunzi waweza kupatiwa kadi za nambari 51-100 na majina yake ili kuziambatanisha katika makundi. 
  • Mwanafunzi aandike nambari 51-100.
  • Wanafunzi waweza kushirikishwa kupanga upya majina yaliyoparaganywa ya nambari 51-100.
  • Mwanafunzi atunge sentensi akitumia nambari 51100.

Mwanafunzi aweza kuonyeshwa vibonzo vikihesabu  hadi 100 kwenye tarakilishi.

                MASWALI DADISI

  1. Unaweza kuandika nambari zipi?
  2. Unaweza kutumia nambari gani kati ya 51-100 katika sentensi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.

Uhusiano na masomo mengine: 

Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali 

Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji  uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake

kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma hadithi 
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti 
  • ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *