Please Limited time Offer!

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua matumizi ya kikomo (.) katika kuimarisha mawasiliano,  
  2. kuakifisha sentensi kwa kutumia kikomo(.) katika kuimarisha uandishi bora,
  3. kuzingatia kikomo (.) anaposoma kifungu na sentensi  ili kuimarisha usomaji bora,
  4. kuthamini matumizi ya kikomo (.) katika mawasiliano. 

              MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi asome sentensi zenye kikomo (.) katika vikundi.
  • Mwanafunzi aakifishe sentensi fupi kwa kutumia kikomo (.).
  • Mwanafunzi aandike sentensi  ukitumia kikomo (.).

                MASWALI DADISI

  1. Unajua alama zipi za kuakifisha?
  2. Je, kikomo (.) huwekwa wapi katika sentensi?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawasiliano na ushirikiano – kushirikiana pamoja darasani ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

elimu ya kudumisha maendeleo: elimu ya maswala ya fedha: kujua kuratibu shughuli za kila siku.

Uhusiano na masomo mengine: 

Mathematics Activities, Environmental Activities na English Activities

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  kuzingatia ratiba ya shule inayoonyesha shughuli za miezi mbalimbali 

Nyimbo na mashairi kuhusu miezi ya mwaka.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji  uzalendo (katika kukumbuka miezi na siku za sherehe za kitaifa).

Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kushiriki katika kuratibu shughuli zinazoendeshwa katika jamii.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuhakiki matamshi ya sauti mbili zinazotamkwa pamoja
  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa miezi ya mwaka na tarakimu katika mawasiliano
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kikomo katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kufuatilia mwandiko wake

kuchunguza anavyotumia lugha katika masimulizi.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti kwa haraka na ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka kwa ubunifu
  • anasoma hadithi kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo kila siku
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko na hati nadhifu na kwa haraka.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka sauti ipasavyo
  • anasimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka 
  • anasoma hadithi kwa ufasaha
  • anafahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa mtiririko na hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti ipasavyo
  • anasimulia baadhi ya hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma hadithi 
  • anafahamu baadhi ya hadithi aliyosoma na kusomewa
  • anaandika baadhi ya sentensi akitumia kikomo 
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka.

 Mbali na Matarajio

Mwanafunzi;

  • anatamka baadhi ya sauti 
  • ana changamoto katika kusimulia hadithi zinazojumuisha miezi ya mwaka
  • anasoma baadhi ya hadithi japo bila ufasaha ufaao
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa
  • ana changamoto katika kuandika sentensi akitumia kikomo
  • ana changamoto katika kuandika kisa.

This is paragraph 2 for posts without the target word.

By Depa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *