Download All Documents- (Ksh 299) Full Day
Hurry during this Offer

CBC Grade 3 Kiswahili Curriculum Designs-7.0-DUKANI-Mada ndogo-7.1-Msamiati

MATOKEO MAALUM YANAYOTARAJIWA

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:-

  1. kutambua msamiati wa dukani ili kuutumia katika mawasiliano,
  2. kusoma maneno yanayohusiana na shughuli za dukani ili kujenga usomaji bora,
  3. kueleza maana ya msamiati wa dukani ili kuimarisha stadi ya

kuzungumza,

  • kutumia msamiati wa dukani katika sentensi sahihi ili kuimarisha stadi ya kuzungumza,
  • kuandika maneno yanayohusiana na uuzaji na ununuzi ili kuimarisha stadi ya kusoma,
  • kuthamini shughuli za biashara.

MAPENDEKEZO YA SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI 

  • Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na shughuli za dukani kwa kutumia kadi za maneno kama vile nunua, uza, bei, kilo, mnunuzi, mwuzaji, hasara, faida, pesa, baki, sarafu na noti.
  • Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu maana ya maneno yanayohusiana na shughuli za dukani kwa kutumia picha au michoro.
  • Mwanafunzi atunge sentensi sahihi kwa kutumia msamiati wa dukani.
  • Mwanafunzi aweza kutazama video kuhusu uuzaji na ununuzi.
  • Wanafunzi washiriki katika majadiliano kuhusu umuhimu wa kufanya biashara wakiwa kwenye vikundi. 

MASWALI DADISI

  1. Mtu anayenunua kitu dukani huitwaje?
  2. Mtu anayeuza dukani huitwaje?

Pesa unazorudishiwa  unaponunua kitu dukani huitwaje?

Umilisi wa kimsingi unaokuzwa: 

mawisiliano na ushirikiano – wanafunzi washiriki katika vikundi ujuzi wa kidijitali – matumizi ya teknolojia katika kujifunza ubunifu – unadhihirishwa na usimulizi na utungaji wa sentensi.

Uhusiano na masuala mtambuko: 

Elimu ya maendeleo endelevu: elimu ya maswala ya kifedha katika ujuzi wa kutumia pesa vizuri.

stadi za maisha – Kuwa na ujasiri wa kwenda na kufanya maamuzi mwafaka ya ununuzi.

Uhusiano na masomo mengine: Mathematics Activities na English Activitites.

Mapendekezo ya shughuli zingine zilizoratibiwa za ujifunzaji:  

kushiriki katika maigizo ya shughuli za dukani shuleni kushiriki katika majadiliano kuhusu bidhaa zinazopatikana dukani.

Uhusiano na Maadili: 

uwajibikaji Kuweza kuwa mwadilifu katika matumizi ya pesa dukani.

ushirikiano – Kufanya kazi katika vikundi.

 Mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji: kuweza kutumwa dukani na wazazi na kutumia pesa inavyofaa.

Mapendekezo ya Tathmini:

  • kuchunguza anavyotumia msamiati wa dukani katika mawasiliano 
  • kuchunguza anavyotumia alama ya kuuliza katika mawasiliano
  • kuchanganua anavyojibu maswali ya kusema na ya kuandika
  • kuchunguza ufahamu wake wa hadithi aliyosoma au kusomewa
  • kuhakiki anavyosoma na kusimulia hadithi

• kufuatilia mwandiko wake.

Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

Kuzidisha Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua na kutumia msamiati wa dukani ipasavyo
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ubunifu na ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha na ukakamavu
  • anafahamu kwa wepesi anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi kila inapohitajika
  • anaandika kisa kwa ubunifu, mtiririko, kwa hati nadhifu na kwa kasi ifaayo.

 Kufikia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua msamiati wa dukani
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anasoma maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani kwa ufasaha
  • anafahamu anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika maandishi
  • anaandika kisa kwa mtiririko na kwa hati bora.

 Kukaribia Matarajio

Mwanafunzi,

  • anatambua baadhi ya msamiati wa dukani.
  • anasimulia kisa kuhusu shughuli za dukani
  • anasoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • anafahamu  baadhi ya mambo anayosoma au kusomewa
  • anatumia alama ya kuuliza katika baadhi ya sentensi
  • anaandika kisa kwa hati zinazosomeka. 

Mbali na Matarajio

Mwanafunzi,

  • ana changamoto katika kutambua baadhi ya msamiati wa dukani
  • ana changamoto katika kusimulia kisa kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kusoma baadhi ya maneno, sentensi na hadithi kuhusu shughuli za dukani 
  • ana changamoto katika kufahamu hadithi aliyosoma au kusomewa
  • ana changamoto katika kuakifisha sentensi kwa kutumia alama ya kuuliza
  • ana changamoto katika kuandika kisa kuhusu mada aliyofunzwa. 

Leave a Comment